Spika wa Bunge, Job Ndugai akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Dodoma, kamati ya ujenzi wa Shule wakati walipotembelea na kujionea ujenzi wa Shule ya Wasichana ya Bunge ya kidato cha Tano na Sita iliyopo Kikombo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mhe. Patrobas Katambi, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Ndg. Godfrey Kunambi, Katibu wa Bunge, Ndg. Stephen Kagaigai, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Dkt. Binilith Mahenge na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Ndg. Maduka Kessy. 
Spika wa Bunge, Job Ndugai (wa pili kulia) pamoja na viongozi wa Mkoa wa Dodoma wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Dkt. Binilith Mahenge (katikati) wakimsikiliza Msimamizi Mshauri wa Majengo ya Shule ya Wasichana ya Bunge ya kidato cha Tano na Sita, Ndg. Howard Fuka tukio lililofanyika leo Kikombo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma. Wengine ni kamati ya ujenzi wa Shule ya Wasichana ya Bunge.
Spika wa Bunge, Job Ndugai (katikati) akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Dkt. Binilith Mahenge (kushoto) pale viongozi wa Mkoa wa Dodoma walipokagua na kujionea ujenzi wa Shule ya Wasichana ya Bunge ya kidato cha Tano na Sita iliyopo Kikombo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma. Wa pili kulia nyuma ni Katibu.
(PICHA NA OFISI YA BUNGE)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...