Mkurugenzi Mkuu wa shulesoft, Efraim Swilla akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa kutamburisha huduma ya bure kwa wanafunzi wa shule za awali, shule za msingi pamoja na shule za sekondari kwaajili ya kujisomea notes(waraka) wakiwa nyumbani kwa kipindi hiki ambacho wamefunga shule kwaajili ya ongezeko la mripuko wa virusi vya COVID 19.
Na Avila Kakingo, globu ya jamii
TAASISI isiyo ya kiserikali ya Shulesoft hapa nchini yaanza kutoa elimu kwanjia ya mtandao ili kusaidia wanafunzi kuendelea na masomo wakiwa nyumbani.
Hii ni kutokana na Dunia na nchi yetu inapitia wakati mgumu wa mapambano dhidi ya Virusi vya COVID 19 yaliyopelekea kusimisha shughuli nyingi za mikusanyiko kwenye Jamii hasa elimu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Machi 25,2020, Mkurugenzi Mkuu wa ShuleSoft, Efraim Swilla amesema kuwa Elimu ni mojawapo ya tasnia mahsusi inayopitia wakati Mgumu kupelekea Serikali kutangaza kufunga Shule zote, ikiwa ni moja ya hatua ya kuzuia kusambaa kwa maambukizi ya virusi vya COVID-19.
"Kwa kulitambua hilo Sisi Vijana Wazalendo na wenye kuiunga mkono Serikali kwenye sekta ya elimu nchini tumebuni njia mbadala kwa kuongeza mfumo mpya kwenye uwanda wetu wa shuleSoft ili kufanikisha Wanafunzi wanaendelea kujifunza wakiwa Nyumbani kwa njia ya mtandao." amesema Swilla.
Amesema mfumo wa ShuleSoft ni uwanja mpana unaoaminika kwa Matumizi ya kufuatilia Uendeshaji wa Shule, Maendeleo ya Mwanafunzi kimahudhurio, Ufaulu na hata kulipia Karo shuleni.
"Program hii inatumiwa na shule zaidi ya 300 na ina Watumiaji wasiopungua Laki moja (100,000) lakini Tanzania ni kubwa, na ina Shule zaidi ya 20,000 na Wanafunzi zaidi ya Milioni kumi hivyo ili kutanua wigo, tumeamua kutoa Mafunzo kupitia Mtandao bila malipo kwa Wanafunzi wote Tanzania kipindi hiki hadi hali itapokua shwari." Amesma Swilla.
Amesema kuwa Kwa shule za binafsi wanaotaka kujiunga watajaza taarifa zao kwenye mtandao wa shulesoft.co.tz na kuunganishwa moja kwa moja na wanafunzi wa Shule za Serikali tayari wametengeneza Mfumo wa moja kwa moja unayofahamika kama jifunze.shulesoft.com
Hivyo Swilla amesema kuwa wanafunzi wote watakapo ingia ndani watakutana na vipindi vitavyokua vinarushwa mubashara na walimu mbalimbali ambao watapenda kujitolea kufundisha wanafunzi na kujibu maswali yao.
Pia kupitia ShuleSoft wanafunzi watapata vitabu mbalimbali, notisi (waraka) pamoja na Majaribio/Mitihani ya kujipima ambayo imewekwa na itaendelea kuwekwa na Walimu mbalimbali watakao jitolea.
"Kampuni,Taasisi au Mtu yeyote mwenye programu itayoweza saidia kutoa elimu kipindi hiki, tunaomba awasiliane nasi tuweze kuunganisha kusaidia taifa".
"Hata hivyo Programu hii itatolewa bure kipindi hiki ambacho Mwanafunzi wapo likizo hawatolipia gharama yeyote." Amesema swilla.
Hivyo wametoa wito kwa watu, Makampuni, Serikali na Taasisi mbalimbali zitazopenda kuunga mkono kuhakikisha swala hili linafanikiwa kwa ufasaha na kila mwanafunzi anapata elimu akiwa nyumbani bila gharama yeyote.
Licha ya hilo wametoa rai kwa wazazi wa wanafunzi kuchangia kwa chochote anachoweza mtu ili kupunguza gharama za uendeshaji na usimamizi wa mtandao wa shulesoft.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...