KUFUATIA Jeshi la Magereza nchini kuzuia huduma za watu kwenda gerezani kusalimia mahabusu kwa sababu ya kuepuka maambuzi ya ugonjwa wa Corona, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema itaruhusu mawakili wa kujitegemea kuongea na wateja wao kupitia video conference endapo watawasilisha maombi maalumu.

Hakimu Mkazi  Mwandamizi, Mfawidhi wa mahakama hiyo Godfrey Isaya amesema hayo leo Machi 25, 2020 alipokuwa akisiliza kesi ya uhujumu uchumi namba 8 ya mwaka 2020 kwa njia ya video conference.

Hatua hiyo imekuja baada ya mshtakiwa Geofrey Urio kuomba mahakama hiyo iwasaidie namna ya kuonana na ndugu zao au mawakili  ili waweze kujua nini kinaendelea katika kesi zao.

"Mheshimiwa kesi yetu inaweza kuisha kwa kufanya makubaliano na DPP (pre bargaining) tunaomba kupata mawasiliano na ndugu zetu japo mmoja tu ili tuweze kubageni na pia tuweze kupata nafasi ya kuongea na mawakili wetu." Alidai Urio

Pia wakili wa Utetezi, Hakika Nzige amedai kuwa wamekuwa wakipata changamoto ya kuona na wateja wao ambao wako gerezani kwani alipoenda gerezani  alikutana na tangazo kwamba hakuna mtu anayeruhusiwa kwenda kuingia gerezani hapo si wakili wala watumishi wa kiroho, hivyo ameomba mahakama iangalie ni namna gani wanasheria/ mawakili wanaweza  kujadiliana na wateja wao.

Akijibu hoja hiyo Hakimu Isaya amesema wataweka utaratibu wa jinsi ya kufanya ili washtakiwa waweze kuwasiliana na mawakili wao kwa kupitia njia hiyo ya video conference haswa kabla ya mahakama kuanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...