SHIRIKAla Uwakala wa Meli Tanzania Mkoani Tanga (TASAC) limetoa wito kwa vyombo vya usafiri vinavyofanya kazi zake majiniambayo havijakaguliwa na kupata cheti cha ubora kutokwenda majinikufanya shughuli zake.

Agizohilo lilitolewa leo na Afisa Mfawidhi wa Shirika hilo Mkoani
Tanga Captain Christopher Shalua wakati akizungumza na mwandishi wa habari ofisini kwake.

Alisemakwamba wao wanatoa wito kwa vyombo vya majini kwa kipindi hiki cha masika vyombo ambavyo havijakaguliwa na kupata cheti cha ubora haviruhisiwi kwenda majini. Afisa Mfawidhi huyo alisema pia kwa kipindi hicho vyombo vyote vilivyopata vyeti vya ubora ni vizuri kuchukua tahadhari kuhakikisha vifaa vyote vya umuhimu ikiwemo pampu za kutolea maji yaliyoingia kwenye chombo zinafanya kazi na zipo.

Aidhaalisema kwa vyombo ambavyo na vyombo havitakuwa
na vifaa vitakavyostahili kuruhusu kwenda majini wanavitaka visienda kufanya shughuli zozote majini kwa kuchukua tahadhari.Tunatoa
rai kwa vyombo vizingatia maelelezo hayo kwa sababu kipindi cha masika
kinaambatana na hali mbaya ya hewa mawimbi makubwa pamoja na mvua ambazo zinasababisha maji kuingia kwenye chombo na kusababisha uzito”Alisema

Alisemakwamba hivyo kama uwezo wa kutoa maji kwenye chombo utakuwa ni mdogo itakuwa rahisi kuzama na hivyo tunatoa wito kwa vyombo vyote hasa kwa uvuvi maelekezo hayo yazingatiwe.

Hatahivyo aliwataka watendaji wa serikali za vijiji na mitaa maeneo ya vyombo vya uvuvi,mizigo vinapotoka kwenye maeneo yao vimekaguliwa na kupatiwa cheti cha ubora na idadi ya vifaa vya uokozi maalumu baharini kulingana na idadi ya wafanyakazi waliopo kwenye chombo hicho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...