Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu, Semistocles Kaijage akizungumza wakati wa mkutano na Viongozi wa Vyama vya Siasa kuhusu mafanikio ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya Kwanza kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Nec, Dkt.  Wilson Charles Mahera
Baadhi ya viongozi  wa Vyama vya Siasa na wadau wengine wakisikiliza kwa makini wakati Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Kaijage akihutubia katika mkutano huo.

Mkurugenzi wa NEC, Dkt.  Wilson Charles Mahera akifafanua jambo wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya viongozi wa Vyama vya Siasa wakichangia mawazo wakati wa majadiliano katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Habari na Elimu ya Mpiga Kura wa NEC, Giveness Aswile akijibu maswali kuhusu umuhimu wa elimu na jinsi ya kuwapatia taarifa mbalimbali wananchi kuhusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.
 Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini Tanzania, John Shibuda akitoa maoni na ushauri kwa Nec na Serikali wakati wa majadiliano katika mkutano huo.





ZAIDI ya Wapiga Kura milioni 30 wamehakiki taarifa zao Awamu ya Kwanza ya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.

Taarifa hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Mstaafu Kaijage wakati wa mkutano na Viongozi wa Vyma vya Siasa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.

 Amesema kuwa,Tume imekamilisha zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la WapigaKura Awamu ya kwanza nchi nzima, kwa mafanikio. Zoezi hili lilianza tarehe 18 Julai, 2019 katika Mikoa ya Kilimanjaro na Arusha na kukamilika 23 Februari, 2020  katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Mwenyekiti huyo wa NEC, amefafanua kuwa,Kabla ya kuanza uboreshaji, Tume kwakutumia taarifa za Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), ilifanya makadirio ya Wapiga Kura wapya watakao andikishwa. Makadirio hayo ya uandikishaji yalikuwa ni asilimia 17 ya Wapiga Kura walioandikishwa mwaka 2015 ambao ni Milioni ishirini na tatu, laki mojasitini na moja elfu, mia nne na arobaini (23,161,440). 

Amesema kuwa, walifanya uchambuzi wa taarifa za zoezi la Uboreshaji kwa Awamu ya Kwanza unaonesha kwamba, Wapiga Kura wapya walioandikishwa ni Milioni saba, arobaini na tatu elfu, mia mbili arobaini na saba (7,043,247) sawa na asilimia 30.41 ya Wapiga Kura walioandikishwa mwaka 2015. Idadi hii imezidi matarajio na makadirio ya awali kwa asilimia 13.41. 
Ametaja Wapiga Kura waliojitokeza kuboresha taarifa zao ni  Milioni tatu, laki mbili,ishirini na tano elfu, mia saba na sabini na nane (3,225,778) ambayo ni sawa na asilimia 13.93 ya Wapiga Kura walioandikishwa mwaka 2015. Aidha, idadi ya Wapiga Kura Elfu kumi na sita, mia saba na saba (16,707) sawa na asilimia 0.07 ya Wapiga Kura walioandikishwa mwaka 2015, waliondolewa kwenye Daftari kwa sababu wamefariki na wengine kupoteza sifa.

Hata hivyo, Jaji mstaafu Kaijage amesema kuwa,Idadi hii ya Wapiga Kura milioni 30 inaweza  kubadilika baada ya kukamilika kwa zoezi la uhakiki na uchakataji wa taarifa za Wapiga Kura endapo watabainika waliojiandikisha zaidi ya mara moja.

Mambo mengine aliyozungumza nao; ni taarifa yakuwepo kwa zoezi la Uwekaji wazi wa Daftari hilo, na kuwapa taarifa ya maandalizi ya zoezi la uboreshaji wa Daftarila Kudumu la Wapiga Kura Awamu ya  Pili.

Pia,alitumia fursa hiyo kuwashukuru kwa dhati Viongozi wa Vyama vya Siasa, kwa namna ambavyo  wametoa ushirikiano kwa Tume wakati  wote wa zoezi la Uboreshaji wa Daftari Awamu ya Kwanza. Aliwaomba waendelee kutoa ushirikiano huo katika michakato inayoendelea na kwamba Tume inaamini kuwa mafanikio ya mazoezi inayoyaratibu na kuyasimamia yanatokana na ushiriki wa Wadau wa Uchaguzi hasa  ninyi wa Vyama vya Siasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...