Waziri wa  Maliasili  na  Utalii, Dkt.  Hamisi Kigwangalla, leo amekutana na viongozi wa Wilaya ya Ngorongoro, Viongozi wa Baraza la Wafugaji Ngorongoro na Uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, kujadili utaratibu wa usimamizi wa fedha zinazotolewa na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kwa ajili ya Baraza la Wafugajji na miradi inayotekelezwa katika Tarafa ya Ngorongoro .

Fedha hizo sasa zitapelekwa kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro  kutekeleza shughuli zilezile zilizokuwa zinatekelezwa na Baraza la Wafugaji Ngorongoro.

Mkutano huo uliofanyika  kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Swagaswaga, umehudhuriwa na Naibu Waziri Wizara ya Maliasili na Utaliii Mhe. Constantine  Kanyasu, Mbunge wa Ngorongoro  na Naibu Waziri wa Elimu,  Sayansi, na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof. Adolf Mkenda ,  Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Bw. Rashid Mfaume Taka na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Maurus Msuha.

Wengine waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Prof. Abiud Kaswamila, Kamishna wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Dkt. Freddy Manongi, Meneja wa Maendeleo  ya Jamii wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro,  Bw. Fedes Mdala.  na Mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji Ngorongoro,  Bw. Edward Maura.
Kamishna wa Uhifadhi, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Dkt. Freddy Manongi, akifafanua jambo wakati wa mkutano wa kujadili utaratibu wa usimamizi wa fedha zinazotolewa na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kwa ajili ya Baraza la Wafugajji na miradi inayotekelezwa katika Tarafa ya Ngorongoro .

 Waziri wa Maliasili na Utaliii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akizungumza wakati wa mkutano na viongozi wa Wilaya ya Ngorongoro, Viongozi wa Baraza la Wafugaji Ngorongoro na Uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kuhusu utaratibu wa usimamizi wa fedha zinazotolewa na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kwa ajili ya Baraza la Wafugajji na miradi inayotekelezwa katika Tarafa ya Ngorongoro . Kushoto kwa Waziri Kigwalla ni Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda, na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Prof. Abiud Kaswamila.


 Mwenyekiti wa Baraza la Wafugaji Ngorongoro, Bw. Edward Maura ( wa kwanza kulia) akizungumza  wakati  wa mkutano wa kujadili utaratibu wa usimamizi wa fedha zinazotolewa na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kwa ajili ya Baraza la Wafugajji na miradi inayotekelezwa katika Tarafa ya Ngorongoro .
 Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof.  Adolf Mkenda  akizungumza wakati wa mkutano  na viongozi wa Wilaya ya Ngorongoro, Viongozi wa Baraza la Wafugaji Ngorongoro na Uongozi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kuhusu utaratibu wa usimamizi wa fedha zinazotolewa na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kwa ajili ya Baraza la Wafugajji na miradi inayotekelezwa katika Tarafa ya Ngorongoro . Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Prof. Abiud Kaswamila.
 Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Prof. Adolf Mkenda,  akimkaribisha Waziri wa Wizara ya Maliasili na Utaliii Dkt. Hamisi Kigwangalla kwenye kikao cha kujadili utaratibu wa usimamizi wa fedha zinazotolewa na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kwa ajili ya Baraza la Wafugajji na miradi inayotekelezwa katika Tarafa ya Ngorongoro . kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano  wa Swagaswaga kwenye ofisi ndogo za Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dodoma .
Meneja wa Maendeleo  ya Jamii wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro  Bw. Fedes Mdala akitoa maelezo wakati wa mkutano wa kujadili utaratibu wa usimamizi wa fedha zinazotolewa na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kwa ajili ya Baraza la Wafugajji na miradi inayotekelezwa katika Tarafa ya Ngorongoro .

Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii,  Dkt. Maurus Msuha akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro  ( kutoka kulia ) ni   Meneja wa Mipango na Uwekezaji wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Bw. Needpeace Wambuya,  Mhasibu Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Bw. Mathew Mkunda na 
Meneja wa maendeleo ya Jamii wa Hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro, Bw. Fedes Mdala  kabla ya mkutano  huo kuanza.
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Bw. Rashid Mfaume Taka, akizungumza  na  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Prof. Abiud Kaswamila ( aliye katikati) na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Maurus Msuha ( Kushoto) mara tu banda ya kuwasili kwa ajili ya mkutano  wa  kujadili utaratibu wa usimamizi wa fedha zinazotolewa na Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro kwa ajili ya Baraza la Wafugajji na miradi inayotekelezwa katika Tarafa ya Ngorongoro .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...