Na Jusline Marco-Arusha

Kesi namba 5,ya mwaka 2020 ya mauaji inayomkabili Mkami Shirima mwenye umri wa miaka 30,kwa kumuua Salome Zakaria mwenye umri wa miaka 18 ambaye ni msaidizi wa kazi za ndani mnamo Machi 6 mwaka huu imeahirishwa Hadi tarehe 8 April mwaka huu.

Kwa upande wake wakili wa serikali Penina Joakimu  amesema kuwa kutokana na upelelezi kutokamilika ameiomba mahakama kupangiwa siku  nyingine.

Akizungumza hakimu mkazi mfawizi wa mahakama ya wilaya Arumeru,Amalia Mushi alisema kesi  hiyo itatajwa tena mnamo April 8 mwaka huu huku mshitakiwa akiwa bado yupo mahabusu katika gereza la kisongo Mkoani Arusha.

Licha yakuwa mshtakiwa huyo  akiwa anakabiliwa na kesi ya mauaji  pia anakabiliwa na kesi ya pili ya usafirishaji wa madawa ya kulevya namba 428 ya mwaka 2019 ambapo inadaiwa yeye na mwenzie aliyefahamika kwa jina la Elias Lairien  kwa kusafirisha madawa ya kulevya aina ya mirungi  huku wakijua ni kinyume Cha sheria.

Akizungumza mahakama ya hakimu mkazi wa  Arusha Gwantwa Mwankuga amesema kuwa kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 8 Aprili kwasababu upelelezi bado  haujakamilika wanasubiri ripoti kutoka kwa mkemia mkuu.

Awali Kesi hiyo ilitajwa kwa Mara ya Kwanza tarehe 24 mwezi 9 mwaka 2019 kwa kosa la kukamatwa na madawa hayo aina ya mirungi kiasi Cha kilogramu 2.95 huko maeneo ya mianzini Mkoani Arusha.

Mshtakiwa wa mauaji ya mfanyakazi wake wa Ndani Mkami Shirima(30)Mkazi wa Sakina Arusha akifikishwa tena katika mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Arumeru akikabiliwa na shitaka la mauaji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...