James Mwanamyoto - Dodoma
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, katika kuboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma bora kwa wananchi, imepokea vitendea kazi vya kielektroniki toka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Umoja wa Mataifa (UNDP).

Vitendea kazi vilivyopokelewa ni Kompyuta saba (7), “printer” 10 na kompyuta mpakato tatu (3) vyenye thamani ya shilingi 45,919,500/=.

Akipokea vitenda kazi hivyo leo toka kwa Bw. James Bwana, Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu, Mkoa wa Shinyanga, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro amemshukuru kwa jitihada zake za kuwezesha upatikanaji wa vitendea kazi hivyo toka UNDP. Awali, James Bwana alikuwa Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Ushirikiano wa Kimataifa, Ofisi ya Rais, Utumishi.

“Nakupatia kompyuta mpakato moja itakayokuwezesha kutekeleza majukumu yako ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wako katika upatikanaji wa vitendea kazi hivyo.” Dkt. Ndumbaro amesisitiza.

Aidha, Dkt. Ndumbaro ameishukuru UNDP kwa kutoa vitendea kazi hivyo vitakavyosaidia kuongeza ufanisi wa kiutendaji kwa watumishi wa ofisi yake.

Kwa upande wake, Bw. Bwana, amemshukuru Dkt. Ndumbaro kwa kumpatia ridhaa ya kufanya mchakato wa upatikanaji wa vifaa hivyo toka UNDP kwa lengo la kuboresha utendaji kazi wa Watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
 Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kulia) akimpongeza Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu, Mkoa wa Shinyanga, Bw. James Bwana kwa kuwezesha kupatikana kwa vitendea kazi vya kielektroniki toka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Umoja wa Mataifa (UNDP) mara baada ya Katibu Tawala huyo kukabidhi vitendea kazi hivyo leo katika ukumbi wa Ofisi ya Rais, Utumishi, Mtumba jijini Dodoma.
 Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu, Mkoa wa Shinyanga, Bw. James Bwana akitoa maelezo ya vitendea kazi vilivyotolewa na UNDP kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kulia) katika ukumbi wa Ofisi ya Rais, Utumishi, Mtumba jijini Dodoma leo.
 Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu, Mkoa wa Shinyanga, Bw. James Bwana, akionyesha nyaraka zenye orodha ya vitendea kazi vilivyotolewa na UNDP kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro (kulia).
 Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi, Ofisi ya Rais, Utumishi, Bw. Victor Ngole, akipokea nyaraka leo toka kwa Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala na Rasilimaliwatu, Mkoa wa Shinyanga, Bw. James Bwana zinazoonyesha orodha ya vitendea kazi vilivyotolewa na UNDP. Anayeshuhudia ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro.

Vitendea kazi vya kielektroniki vilivyotolewa na UNDP kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa watumishi wa watumishi wa Ofisi ya Rais, Utumishi vikishushwa leo kwa ajili ya makabidhiano rasmi katika ofisi hiyo, Mtumba jijini Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...