Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amewataka wafugaji nchini kuhakikisha kuwa wanachukua tahadhari Juu ya Virusi vya homa ya Mapafu Covid -19 ambavyo vinasababisha Ugonjwa wa Corona.

Akizungumza na wafugaji mara baada ya kutembelea minada ya mifugo katika soko la kimataifa la mifugo lilipo wilayani longido pamoja na mnada wa Meserani,uliopo wilayani monduli mkoani Arusha,Ulega alisema kuwa tahadhari ni muhimu kuchukuliwa na kuhakikisha kuwa wafugaji na wafanyabishara wanawana mikono.

Aidha alisema kuwa Pindi biashara ya mifugo inapofanyika ni vyema kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima ni vyema ambapo amewataka wafugaji kurejea majumbani ili kujikinga na gonjwa hilo.

Katika hatua nyingine naibu waziri Ulega alitembelea kituo cha wizara ya mifugo na uvuvi kilichopo katika boda ya namanga na kuzungumza na maafisa hao,ambapo alisema kuwa serikali imeruhusu biashara kufanuyika kama kawaida hivyo waisaidie serikali katika eneo hilo.

Alisema ni lazima biashara na shughuli za kiuchumi ziendelee ili serikali ipate mapato, huku familia zipate mahitaji yao muhimu.“Hatuwezi kufunga minada hii sababu maisha ya watanzania walio wengi huishi kwa kutafuta mlo a kila siku, hivyo kuzuia minada hii ni sawa na kuataka wafe kwa njaa, sasa hili serikali tumelitafakari ka kina na tumeona haifai kuifunga minada hii,”alisema.

“Ninachosisitiza hapa kwenye minada hii wawepo tu wale wanaouza mifugo na wanaonunua, lakini mkishauziana tu ondokeni mara moja mnadani na sitaki muweke mikusanyiko,”alisema.

Aidha alipongeza minada hiyo kutokana na tahadhari zilizochukiwa ambapo ili kuthubiti mikusanyiko makundi ya wafugaji na wafanyabishara imepungua kwa kiasi kikubwa tangu kulipozuka Ugonjwa huo huku kila anayeingia akinawa mikono kwa maji safi yanayotiririka.

Mkuu wa Wilaya ya Longido, Frack Mwaisumbe,alishukuru serikali kuruhusu wananchi wake kuendelea na minada ya mifugo, sababu ni sehemu ya maisha yao,huku akieleza wazi kuwa hapo awali mnada huo wa longido ulifunngwa kutokana na kuzua taaruki kubwa kwa wananchi mara baada ya mgonjwa wa kwanza wa Corona kutangazwa.


Naibu wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akitembelea Boda ya NAMANGA ambapo Kuna kituo Cha Wizara hiyo ili kutoa maelekezo yake.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akipokea maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe Mara baada ya kufika katika soko la Mifugo ya kimataifa lililopo wilayani humo.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega Akiwa na mbunge wa Monduli Julius Kalanga wa Pili Kulia kwake wakati alipotembelea mnada wa Miserani uliopo wilayani Monduli mkoani Arusha.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akinawa Mikono Kama tahadhari ya Ugonjwa wa Corona katika mnada wa Miserani
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akipokea maelezo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe Mara baada ya kufika katika soko la Mifugo ya kimataifa lililopo wilayani humo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...