Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (wa kwanza kulia) akizungumza na watumishi wa Idara ya Ulaya na Amerika wakati alipowatembelea na kujadililiana nao masuala mbalimbali ya utendaji kazi wa Idara hiyo kwenye ofisi za Wizara zilizopo Chuo Kikuu cha Dodoma, tarehe 31 Machi 2020

Mhe. Waziri Prof. Kabudi akimsikiliza mmoja wa watumishi wa Idara ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakitoa ufafanuzi kuhusiana na utekelezaji wa majukumu ya idara.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi ametembelea Idara na vitengo vya wizarani na kuzungumza na watumishi walioko katika ofisi za wizara kwenye majengo ya Chuo Kikuu cha Dodoma, tarehe 31 Machi 2020.

Prof. Kabudi ametumia nafasi hiyo kuzungumza na mtumishi mmoja mmoja ili kuwafahamu na kuona jinsi wanavyoyafahamu na kutekeleza majukumu yao ikiwa ni pamoja na kuona namna wanavyogeuza changamoto wanazokutana nazo kuwa fursa katika sehemu zao za kazi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...