Waziri wa kilimo Mhe. Japhet Hasunga ameihaidi menejimenti ya Tanzania Horticultural Association (TAHA) ushirikiano katika kukuza tasnia ya horticulture nchini Ahadi hiyo imetolewa na mhe.Hasunga alipotembelea ofisi za makao makuu ya taasisi hiyo zilizoko mkoani Arusha 

Akitoa maelezo mafupi kuhusu tasnia hiyo kwa Mhe. Waziri, Afisa Mkuu Mtendaji wa TAHA Dkt. Jacqueline Mkindi amemweleza waziri jitihada zilizofanywa na taasisi hiyo katika kukuza tasnia ya horticulture tangu kuanzishwa kwakwe mwaka 2004. Aidha Dkt. Mkindi amesema kwa miaka yote licha ya jitihada zinazofanywa na TAHA na manufaa zinazoshuhudiwa na wananchi lakini serikali imekuwa na mchango mdogo kwa kutoitambua tasnia hiyo kama sekta rasmi inayoweza kuwezesha upatikanaji wa ajira na kukuza pato la taifa. 

Dkt. Mkindi amesema horticulture ndiyo kilimo chenye manufaa kwa sasa duniani kwani mazao yake yanauhitaji mkubwa na soko la uhakika. Akitolea mfano wa zao la parachichi, Dkt. Mkindi amesema zao hilo linahitajika kwenye masoko yote dunia na hasa parachichi kutoka Tanzania Amemwomba waziri kupitia wizara ya kilimo kutoa msaada mkubwa hasa katika kusimamia ushindani wa kibiashara kwa kuzingatia kuwa kuna mataifa yanakuja na mbinu chafu ili kudhoofisha biashara hiyo kwa kutambua kuwa Tanzania itanufaika sana. 

 Vile vile Dkt. Mkindi amemwomba Mhe.Waziri kusaidia kusukuma uanzishwaji wa mamlaka ya usimamizi wa tasnia ya horticulture ili kuipa nguvu Zaidi katika kuzalisha na kuongeza pato la taifa, kwani haipewi uzito mkubwa kwa sasa kutokana na kukosekana kwa mamlaka husika ya kusimamia tasnia hiyo. 

 Kwa upande wake Waziri wa kilimo Mhe.Japhet Hasunga, amesema hakuwa na uelewa wa kutosha juu ya tasnia hii hivyo kufanya maamuzi yote kuegemea kwenye takwimu na maelezo kutoka kwa watendaji wa wizara Aidha amesema kwa ufahamu na uelewa alionao juu ya tasnia hiyo atautumia katika kutoa maamuzi yenye tija itakayosukuma mbele kilimo hasa cha horticulture 

 Mhe.Hasunga amesema kuhusu ombi la Dkt.Mkindi kuhusu usimamizi wa soko la nje na kudhibiti propaganda potofu, amemsema serikali kupitia wizara yake itashughulikia jambo hilo kwa unyeti wake. Hata hivyo amesema serikali inashughulikia taratibu kadhaa ili kuwezesha makubaliano ya pande zote za nchi ili kuwezesha kufunguka kwa masoko yatakayofanikisha biashara ya mazao ya horticulture nchini. 

 Akitolea mfano wa soko la Uchina na Arabuni ambayo amesema serikali na makubaliano ya awali(memorandum of understanding) ambayo inahitaji kutimiza baadhi ya masharti machache na maelekezo kadhaa ili kuifanya itumike Mwisho waziri Hassunga ameiomba TAHA kushirikiana na serikali kikamilifu katika kutoa mwongozo na ushauri wa kitaalum kwa kuzingatia kuwa asasi hiyo ndiyo yenye uzoefu na sekta, hivyo kuwezesha sera mpya kutoa dira thabiti kwa ajili ya ustawi wa kilimo hicho nchini.
Waziri wa kilimo Mhe. Japhet Hasunga akilakiwa na Afisa Mkuu Mtendaji wa TAHA Dkt. Jacqueline Mkindi

Afisa Mkuu Mtendaji wa TAHA Dkt. Jacqueline Mkindi akimkaribishaWaziri wa kilimo Mhe. Japhet Hasunga

Waziri wa kilimo Mhe. Japhet Hasunga akiongea
Waziri wa kilimo Mhe. Japhet Hasunga akisindikizwa na Afisa Mkuu Mtendaji wa TAHA Dkt. Jacqueline Mkindi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...