Shirikisho la soka barani Afrika
(CAF) limeahirisha Mashindao ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji
wanaocheza ndani (CHAN) kufuatia kuongezeka kwa maambukizi ya COVID19
(virusi vya corona)
Mashindano hayo yalipaswa kuanza April 04 mpaka April 25 2020 huko Cameroon.
Tanzania ni miongoni mwa timu zilizokuwa zishiriki mashindano hayo ambapo kikosi cha Stars bado kiko kambini
Baada ya uamuzi huo ni wazi kambi
itavunjwa na wachezaji kurejea kwenye timu zao kuendelea na ligi kuu
(kama TFF haitasimamisha ligi)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...