Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji ,Angela Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na watoto wenye ulemavu akikabidhi baadhi ya misaada katika kituo cha kulelea watoto yatima kama picha inavyoonekana
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji ,Angela Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na watoto wenye ulemavu
Waziri Angela Kairuki akikabidhi vifaa mbalimbali kwa watoto pamoja pampers na sabuni pamoja na vyakula katika vituo vya Mama Kevin pamoja na Tumaini children center ambayo ni makao ya watoto.



Na.Vero Ignatus,Same.

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji ,Angela Kairuki atoa misaada katika vituo vya kulelea watoto yatima pamoja cha Rafiki Children Center na kituo cha watoto wenye ulemavu Wilayani Same cha Mama Kevin ikiwa ni njia mojawapo ya kuiwezesha jamii hiyo ambayo imekua ikisahaulika.

Kairuki amekabidhi vifaa mbalimbali kwa watoto pamoja pampers na sabuni pamoja na vyakula katika vituo vya Mama Kevin pamoja na Tumaini children center ambayo ni makao ya watoto.

Aidha amewapongeza walezi wa vituo hivyo kwa kazi kubwa wanaoyifanya ya kulea watoto katika misingi ya maadili mema ,uzalendo na kukua vizuri kiroho ii waweze kuwa na mchango katika jamii licha ya changamoto walizonazo sasa.

Amewataka wakazi wa same kuungana na kujenga utamaduni wa kusaidia watoto yatima walioko katika vituo ili waweze kukua vyema na kulijenga taifa lao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...