Na Vero Ignatus,Killimanjaro.
Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji ,Angellah Kairuki amegawa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Makanye iliyoko wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro lengo ikiwa ni kuwasaidia watoto wa kike wanaotoka kwenye kaya zenye uhitaji waweze kupata msaada huo.
Akikabidhi taulo hizo ,Kairuki amepongeza juhudi za serikali za kutoa elimu bure kwa wanafunzi wote bila kubagua jambo ambalo litawawezesha watoto wa kitanzania kutimiza ndoto zao.
Kairuki amewataka watoto wa kike kujiepusha na vishawishi na mahusiano kabla wa wakati muafaka ili wasikatishe ndoto zao kwa mimba za utotoni.
“Hapa kuna madaktari,mawaziri,wakandarasi hivyo tunaomba msome kwa bidii ili muweze kutimiza malengo yao” Alisema Kairuki

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...