Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii kabla ya kuzindua Kamati hiyo, jijini Dodoma, leo, ambayo itasimamia Utekelezaji wa Sheria ya Huduma kwa Jamii inayotoa fursa kwa wafungwa wa vifungo vidogo kutumikia adhabu hizo kwenye jamii. Pia Waziri huyo ameitaka Kamati hiyo, iweke mikakati zaidi ya kusimamia adhabu mbadala ya kifungo cha nje ili kuondoa msongamano magerezani. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (katikati meza kuu), akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio, alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii kabla uzinduzi wa Kamati hiyo, jijini Dodoma, leo.  
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia), akimsikiliza Katibu wa Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma za Uangalizi, Aloyce Musika, alipokuwa anazungumza kabla ya kabla uzinduzi wa Kamati hiyo, jijini Dodoma, leo. Waziri Simbachawene amezindua Kamati hiyo, ambayo itasimamia Utekelezaji wa Sheria ya Huduma kwa Jamii na kutoa fursa kwa wafungwa wa vifungo vidogo kutumikia adhabu hizo kwenye jamii.  Wapili kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Jaji Zephrine Galeba.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (wanne kushoto), Katibu Mkuu, Christopher Kadio (wanne kulia), Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii, Jaji Zephrine Galeba (watatu kushoto), Katibu wa Kamati, Aloyce Musika (watatu kulia), Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee (wapili kulia), wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati hiyo, jijini Dodoma, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...