
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Rais Mhandisi Joseph Malongo ameongoza watumishi wa Ofisi yake katika
mazishi ya Alazaro Sokoine ambaye ni mtoto Mkubwa wa Hayati Edward
Moringe Sokoine. Mazishi hayo yamefanyika jana Monduli Juu Mkoani Arusha
na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, ndugu, jamaa na
Marafiki.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Balozi
Joseph Sokoine (kushoto) akiweka shada la maua pamoja wanafamilia
katika kaburi la kaka yake mkubwa Alazaro Sokoine. Mazishi yamefanyika
jana Monduli Mkoani Arusha.

Mkurugenzi wa Utawala na usimamizi
wa Rasilimali watu Bi. Emma Lyimo akitoa heshima za mwisho katika
ibaada ya kuaga mwili wa Alazaro Sokoine ambae ni mtoto mkubwa wa Hayati
Edward Moringe Sokoine. Mazishi yamefanyika jana Monduli Mkoani Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...