Mkurugenzi wa Tiba (MOI) Dkt. Samwel Swai (kulia) akipokea baadhi ya vifaa kutoka kwa Meneja wa Kampuni ya EAA Josiah Benedict leo katika viwanja vya (MOI) jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Tiba (MOI) Dkt. Samwel Swai akiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Kampuni ya EAA Josiah Benedict pamoja na baadhi ya wafanyakazi wengine waliohudhuria warsha ya makabidhiano leo katika viwanja vya (MOI) jijini Dar es Salaam

******************************
Kampuni ya EAA Co. Ltd ya nchini Japan imetoa msaada wa viungo bandia vyenye thamani ya Shilingi milioni 80.9 kwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) leo Jijini Dar es Salaam.

Akipokea msaada huo, Mkurugenzi wa Tiba (MOI) Dkt. Samwel Swai amesema kuwa msaada huo utasaidia kwa kiasi kikubwa matibabu ya wagonjwa wenye ulemavu wa miguu naa mikono.

Kwa upande wake Meneja wa Kampuni ya EAA Co. Ltd, Josiah Benedict amesema wameguswa na changamoto zinazowakabili watanzania ndiyo maana wameamua kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli ya kuboresha huduma za afya hapa nchini.

Msaada huo unatokana na juhudi za Ubalozi wa Tanzania Japan kwa kushirikiana na Watanzania waishio nchini Japan.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...