NA
YEREMIAS NGERANGERA….NAMTUMBO.
Bodi ya afya
katika Halmashuri ya wilaya ya Namtumbo
mkoani Ruvuma imeridhishwa na ujenzi wa majengo ya kutolea huduma za afya katika Halmashauri hiyo.
Akiogea
wakati wa majumuisho ya ziara ya kukagua ujenzi wa vituo vya kutolea
huduma za
afya mjumbe wa bodi ambaye pia ni diwani
wa kata ya Magazini bwana Saidi Ligulu alisema bodi ya afya ya wilaya
imeridhishwa na ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za afya
zilizokaguliwa
na bodi hiyo.
Aidha
bwana
Ligulu alimpongeza kaimu mganga mkuu wa wilaya ya Namtumbo bwana Godwin
Lutta kwa kuwaandalia ziara ya kukagua na kujionea ujenzi
wa vituo vya kutolea huduma za afya katika halmashauri ya wilaya ya
Namtumbo ili waweze kuwa wajumbe wazuri kwa wananchi wanaowawakilisha
katika maswala
ya afya.
Hata
hivyo bwana Ligulu alipongeza
ushirikiano uliopo kati ya kamati za ujenzi ,wananchi wanaotoa nguvu zao katika kuhakikisha ujenzi
uafanyika pamoja na uongozi wa Halmashauri katika kuhakikisha ujenzi huo
unakidhi vigezo vilivyowekwa na wizara
ya afya.
Naye Antony
Mbawala mjumbe wa bodi hiyo kutoka katika kata ya Msindo kwa upande wake pamoja na kumpongeza kaimu mganga mkuu kwa
kuwaandalia ziara kujionea ujenzi wa vituo vya afya alidai ziara hiyo
imewafanya watambulike na wahudumu wa vituo vya kutolea huduma za afya na
kuongeza kuwa kitendo hicho kitawarahisisishia wajumbe hao kuhoji mambo
mbalimbali katika vituo vya kutolea huduma za afya bila wasiwasi wowote tofauti
na mwanzo ambapo wahudumu hao walikuwa hawawatambui pale walipotaka kuhoji
mambo katika vituo hivyo.
Wajumbe katika ziara hiyo walikubali kutumia magari
yao binafsi ili kuepuka msongamano katika gari moja la halmashauri ili
kujikinga na maambukizi ya ugonjwa hatari wa Corona.
Ziara ya
wajumbe hao wa bodi ya afya ilikagua
ujenzi wa majengo nane ya hospitali ya wilaya ya Namtumbo ,ujenzi wa Zahanati ya
ukiwayuyu pamoja na ujenzi wa majengo ya
kituo cha afya cha Mtakanini katika kata ya Msindo na kuridhishwa na ujenzi wa
vituo hivyo vya kutolea huduma za afya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...