
Mhe. Bashungwa aliyasema hayo mkoani Kilimanjaro alipofanya ziara katika kiwanda cha cha kuzalisha sukari cha TPC ili kujiridhisha na hali ya uzalishaji viwandani hapa.
Kuna viwanda vinne Kagera sugar, Mtibwa Sugar, Kilombero Sugar na TPC wakati vinabinafsishwa vilipewa malengo ya kuongeza uzalishaji wake.
TPC kilipobinafsishwa mwaka 2007 kilipewa malengo ya kuzalisha tani 75,000 lakini kwa sasa kinazalisha tani 100,000 kwa mwaka.
"Baada ya kutembelea TPC wanawatumia ujumbe viwanda vingine kama Kagera Sugar, mtibwa Sugar, kilombero Sugar kurejea mikataba ya ubinafsishaji ili kujiridhisha kama wanaenda sambamba na mikataba hiyo."
Bashungwa aliongeza kuwa viwanda vya Kagera sugar, Mtibwa sugar na Kilombero kurejea mikataba ya uzalishaji kuna malengo ya serikali, nitapita kuangalia kama mmezingatia mnafuatilia mikataba ya uzalishaji.
"Kama watakuwa wameshindwa kutimiza malengo hayo basi watakuwa wanatukwamisha.
"Mhe Rais Dk John Pombe Magufuri alipoingia madarakani mwaka 2015, aliweka malengo ya kuwa nchi ya viwanda ili tujitegemee katika uzalishaji wa vitu kama sukari."
Mhe Bashungwa aliendelea kusema "viwanda hivi vi
natoa ajira kubwa kwa kinamama na vijana, mfano hapa TPC peke yake wanatoa ajira elfu nne za moja kwa moja achilia mbali zile zinazokuja kutokana na uzalishaji na usafirishaji.
"Endapo viwanda vya kuzalisha sukari vya kagera , Mtibwa na Kilombero vitazingatia mkataba wa uzalishaji basi hakutakuwa na uhaba wa sukari hapa nchini. Tutaachana na masuala ya kuagiza sukari kila mwaka pamoja na upungufu wa bidhaa hiyo.
"Nia ya Serikali ni kuzalisha sukari kwa wingi ili kuuza ndani ya nchi na nje ya nchi katika masoko ya EAC, SADC,COMESA kwa kuwa nchi yetu ni mwanachama wa jumuiya hizo zote".
Aidha amewaonya wafanyabiashara wanaosambaza sukari nchini ambao wanatumia kipindi cha mfungo kuongeza bei ya sukari, kuwa serikali haitawafumbia macho kwa kufanya kitendo hicho.
Ole wenu tukiwabainisha tutawawafutia leseni za biashara ,hamtafanya biashara tena kama mkibainika kupandisha bei ya sukari.
Aliongeza kusema serikali imetoa ukomo wa bei za sukari ya kiwango cha juu si lazima mtu akauza bei hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...