
Marehemu Shah (Bujji) pamoja na tofauti zetu za kisiasa baina yake na familia yetu hususan katika wakati wote wa zile kampeni za kisiasa, bado alikuwa ni mtu mwenye upendo nidhamu utu heshima na uungwana wa hali ya juu hasa kwa wazazi wetu na sisi watoto.Buji alikuwa kaka, rafiki, mtani na kiongozi wetu mstaafu tutamkumbuka siku zote..
Mungu awatie nguvu na awape moyo wa subra ndugu na jamaa na watoto wake wote katika kipindi hiki kigumu...kipekee tunampa pole sana mke wa marehemu Bi. Naila kwa kumpoteza mwenza na baba wa watoto wake..
Mungu awape moyo wa subra na aweke roho ya marehemu kaka yangu rafiki yangu Bujji mahala pema peponi
ILWIR
Omary Ayoub Kimbau
(Kwa niaba ya familia ya Kimbau)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...