Uzalishaji wa Barakoa ukiendelea katika kiwanda Cha Pristine Manufacturing Company Limited.
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kiwanda Cha Pristine Manufacturing Company Limited Kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam Alnoor Lakha wakati waziri huo alipotembea kiwanda hicho.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Akida Khea akizungumza namna wanavyozalisha Vifaa Tiba vya Barakoa na kuwazimeweza kukidhi vigezo vinavyohitajika wakati walipotembelea kiwanda Cha kuzalisha Barakoa zinazozlishwa na kiwanda Cha Pristine Manufacturing Company Limited Kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa akizungumza na waandishi wa Habari wakati alipotembelea kiwanda Cha kuzalisha Barakoa (Face Mask) Pristine Manufacturing Company Limited Kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa akiangalia Barakoa zinazozlishwa na kiwanda Cha Pristine Manufacturing Company Limited Kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa akiwa katika picha ya pamoja wazalishaji wa Barakoa , TMDA,TBS pamoja FCC.
Mkurugenzi Mkuu wa wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Dkt Yusuf Athuman Ngenya akizungumza kuhusiana na Viwango vya ubora wa Barakoa zinazozlishwa na kiwanda Cha Pristine Manufacturing Company Limited Kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV.
Serikali ipo makini kuahakikisha inawalinda wananchi wake dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona hivyo itaendelea kushirikiana na viwanda vyote vinavyozalisha vifaa tiba kwaajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi hivyo pamoja na kuwasaidia changamoto wanazokutana nazo .
Hayo ameyasema Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa alipotembelea kiwanda cha kuzalisha Barakoa (Face Mask) Pristine Manufacturing Company Limited kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam amesema kuwa serikali iliona mbali ya kuhakikisha wananchi wanafanya Kazi huku wananchi wakiendeleea kujikinga na Virusi vya Corona.
Amesema nchi ambazo zimewafungia wananchi wake sasa wanajuta kwani mahitaji ya ugonjwa huo ni mengi.
Akizungumza katika kiwanda hicho Bashungwa amesema kuwa Serikali itahakikisha inatatua changamoto za upatikanaji wa malighafi kwaajili ya kutengenezea vifaa tiba kwaajili ya kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona.
Aidha Bashungwa ameeleza kuwa atakaa na balozi wa India, Balozi wa China na kufanya kila liwezekanalo malighafi ambayo yanatoka katika nchi hizo zinakuja kwa njia ya haraka.
"Zile bidhaa zinazoingia kutoka nje ya nchi nimewaambia wafanyabiashara kwamba pale wanapokwama wawasiliane na wizara yangu tutahakikisha kama ni changamoto ambazo zipo bandarini au TRA na mahali pengine popote tunashirikiana ndani ya serikali kuhakikisha zile bidhaa ambazo hatuzizalishi zinatoka nje basi hazitacheleweshwa ili kuweza kuingia kwenye mzunguko wa usambazaji". Amesema Bashungwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Dkt.Athuman Ngenya amesema kuwa ubora wa viwango kwa vifaa tiba hasa barakoa upo vizuri uliokidhi viwango kwaajili ya kujilinda na maambukizi ya Virusi vya Corona
"Sisi kama TBS shughuli yetu ni kuweka viwango na viwango tayari vipo na hawa ndugu wameshakuja na wameshachukua viwango na vifaa hivi (Barakoa) vimetengenezwa kulingana na viwango". Amesema Dkt.Ngenya.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA), Bw.Akida Khea amesema kuwa kazi kubwa ya Barakoa ni kuzuia maambukizi hivyo mwanzo wanasayansi walishauri Barakoa itumike kwa watu ambao wanamaambukizi ili wasiweze kuwaambukiza watu wengine lakini Shirika la Afya Duniani limebadili msimamo wake inasemekana kwamba kifaa kinahitajika kila mtu atumie kwani maambukizi ya Virusi vya Corona yanaambukizwa kwa njia ya hewa sio kwamba ilivyofahamika awali.
Pia Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Kuzalisha Barakoa (Pristine Manufacturing Company Limited), Bw.Alnoor Lakha amesema kuwa kiwanda hicho kinazalisha wastani wa barakoa kati ya elfu 20 mpaka elfu 30 kwa siku.
Pmoja na hayo Bw.Lakha amesema kuwa uhitaji wa Barakoa ni mkubwa kwasasa kulingana na hapo awali ambapo Virusi vya Corona havikuwepo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...