Kampuni ya uajiri
na usimamizi wa rasilimali watu ya BrighterMonday Tanzania imeanzisha programu
iitwayo ‘Umoja Wakati wa Shida’ inayotoa nafasi kwa waajiri (makampuni na watu
binafsi) kutangaza kazi kwenye tovuti yao bure kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo,
wakati ambao taifa linakabiliana na janga la maradhi ya virusi vya Corona.
Kampeni hii
inalenga kuwezesha uendelevu wa juhudi za makampuni na biashara kwa kuziwesesha
kufanya udahili na kuajiri watendaji sahihi ili kuongeza ufanisi wakati na
baada ya nyakati hizi za changamoto.
‘’Kwa miezi mitatu
ijayo, tutatoa fursa kwa taasisi zinazotaka kuajiri wataalamu katika sekta
mbalimbali kote nchini kutangaza bure nafasi za ajira katika tovuti yetu. Hii
itawawezesha hospitali, vituo vya afya na watoa huduma nyingine muhimu walio
mstari wa mbele katika kukabiliana na janga la virusi vya Corona (COVID-19)
kuajiri wataalamu wenye vigezo kamilifu katika kipindi cha muda mfupi’’, anasema Mkurugenzi Mkuu wa BrighterMonday Tanzania, Bi. Reshma
Bharmal-Shariff.
Chini ya programu
hii, waajiri wataweza kuchakata kwa haraka mchakato wa uajiri kwa kutumia mbinu
za kisasa zilizobuniwa na BrighterMonday Tanzania kama vile Zana ya Kupima
Ufanisi wa Waajiriwa ambayo inapima ubora wa mwajiriwa na ujuzi unaohitajika
kwa kazi anayoomba, zana hii hupima zaidi ya kile kilichopo kwenye wasifu (CV)
ya mtahiniwa.
Vilevile, waajiri
wataweza kuangalia alama za mtahiniwa pamoja kulinganisha na mahitaji ya
kitaaluma na kiuzoefu kwa kutumia mfumo wa ufuatilaji wa maombi ya kazi
‘Application Tracking System’ (ATS) wa BrighterMonday Tanzania. Kupitia mfumo
huu, mwajiri ataweza kulinganisha kwa urahisi ubora wa mtahiniwa, ujuzi na
kiwango cha uzoefu.
‘Tupo kwa ajili
yako jana, leo na hata kesho’- Timu ya
BrighterMonday Tanzania inasema.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...