Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee
na Watoto Ummy Mwalimu amesema Tanzania imeanza kupata maambukizi ya Virusi vya
Corona ya ndani kuanzia maambukizi yaliyopatikana tarehe 08/04/2020.
Amesema kuwa tahadhari kubwa inahitajika katika
kuhakikisha kuzuia kuendelea kwa maambukizi ya kijamii itasababisha
kuongezekana kwa kasi ya maambukizi katika jamii.
Ameyazungumza hayo leo jijini Dar es Salaam wakati
wa mkutano na viongozi wakuu wa madhehebu ya dini katika kujadiliana namna ya
kukabiliana na maambukizi ya virusi ya Corona nchini.
Ameongeza kuwa Serikali itatangaza hivi karibuni
wananchi kuchukua tahadhari kwani tafiti zinaonesha virusi vya Corona vinaweza
kusambaa na kuambukizwa kwa njia ya hewa hivyo maelekezo ya kutumia barakoa yatatolewa
ili kuondokana na maambukizi.
“Tafiti zimeonesha kuna uwezekano wa Virusi vya
Corona vinaweza kuenezwa kwa njia ya hewa hivyo tutaleta muongozo wa kuanza kutumia
Barakoa (Mask) kwa jamii ili kuziua maambukizi kuenena kwa njia ya hewa”
alisema
Aidha amewataka viongozi wa dini kutoa rai kwa
wazazi na walezi kuwalinda watoto kutowaruhusu Watoto kuzurula na kuhangaika ovyo
mitaani ili kupunguza uwezekano wa kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya
Corona.
“Imani ya watanzania wengi kufikiri kuwa hatuwezi
kupata maambukizi ni suala sahihi tunaweza kupata maambukizi kama watu wengine
wanavyopata” alisema.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii
Dkt. John Jingu amesema kuwa viongozi ni watu muhimu katika kuleta mabadiliko
katika Jamii yetu kwani wanasikilizwa zaidi na waumini katika sehemu za ibada.
Ameongeza kuwa lengo ni kuwashirisha viongozi wa
kidini katika kuhakikisha wanatimiza wajibu wao katika kuhakikisha maambukizi
ya virusi vya Corona yanatokomea nchini.
"Viongozi wa kidini ni watu muhimu sana
katika mapambano katika kuondokana na maambukizi ya Virusi vya Corona nchini
tunaomba mtusaidie katika hili" alisema
Naye Mkurugenzi wa Shirika la World Vision Gilbert
Kamanga amewaomba vingozi wa dini kutofanya suala la virusi vya Corona kuwa la
kisiasa bali waunganishe nguvu pamoja ili kuondokana na maambukizi ya virusi
vya Corona.
Ameongeza kuwa jamii inatakiwa kupewa elimu kila
mahali ikiwemo katika nyumba za ibada ambapo watu wengi ukusanyika pamoja
kuabudu itakuwa sehemu sahihi kufikisha ujumbe kuhusu kuondokana na maambukizi
ya virusi vya Corona.
"Viongozi wetu wa dini nawaomba tushikamane
katika hili kwani virusi vya Corona ni hatari sana lakini tukisimama pamoja
hakika tutafanikiwa katika kutokomeza virusi vya Corona" alisema
Akitoa salam za mkoa wa Dar es Salaam Mganga Mkuu
wa Mkoa huo Dkt. Rashid Mfaume amesema mkoa umejidhatiti katika kupambana kwa
kuenea na maambukizi ya Virusi vya Corona mkoani humo kwa kuzingatia maelekezo
yanayotokea na wataalam wa Afya na
Serikali kwa ujumla.
Naye Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhaji
Musa Salum amesema janga la Corona ni kubwa na kama watu wa imani tunaamini katika
kumuonba Mwenyezi Mungu na tunaamini litatokomea.
Pia amemshukuru Rais John Magufuli kuendelea
kuruhusu ibada kuendelea katika kama kawaida ni jambo ambalo litasaidia
kuzidisha maombi katika kupambana na Virusi vya Corona.
Mkutano huu kati ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na viongozi wakuu wa madhehebu ya
dini umekuja wakati Tanzania ikiendelea kupambana na maambukizi ya virusi vya
Corona huku ikiwa na jumla ya watu 25 waliombukizwa virusi hivyo.
aziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na viongozi wa dini kuhusu mapambano dhidi
ya maambukizi ya Virusi vya Corona nchini katika Mkutano uliofanyika leo jijini
Dar Es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya- Idara Kuu ya Maendeleo
ya Jamii Dkt. John Jingu akielezea jinsi Wizara inavyoshirikiana na wadau
katika mapambano dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Corona katika Mkutano kati
ya Wizara(Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) na viongozi wa Dini jijini Dar Es
Salaam.
Mkurugenzi wa Shirika la World Vision
Gilbert Kamanga akielezea jinsi Shirika hilo linavyoshirikiana na Serikali
katika mapambano dhidi maambukizi ya Virusi vya Corona katika Mkutano kati ya
Wizara(Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) na viongozi wa Dini jijini Dar Es Salaam.
Baadhi ya viongozi wa kidini wakifuatilia
mada zilizokuwa zikitolewa katika Mkutano kati yao na Wizara ya Afya- Idara Kuu
ya Maendeleo ya Jamii uliofanyika leo jijini Dar Es Salaam.Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
WAMJW
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...