Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
WAKATI
vizuizi vikipungua nchini China ikiwa ni sehemu ya kupambana na virusi
vya Corona (Covid -19) klabu moja ya mpira wa miguu nchini humo
imeeleza nia yake ya kurudisha mambo katika hali ya kawaida.
Klabu
ya Guangzhou Evergrande imetangaza kuanza kazi ya kujenga uwanja wa
mpira utakaobeba watazamaji 100,000, na utakua uwanja mkubwa zaidi
ulimwenguni.
Imeelezwa
kuwa uwanja huo umejengwa katika umbo la ya aina ya lotus utagharimu
dola za kimarekani Bilioni 1.7 (Yuan Bilioni 12) na unategemewa
kumalizika mwishoni mwa mwaka 2022.
Aidha
imeelezwa kuwa kazi ilianza Alhamisi iliyopita, huku lengo la kujengwa
kwa uwanja huo ikielezwa ni kuweka alama mpya ya kiwango cha juu duniani
ambapo uwanja huo umelinganishwa na jumba la Opera la Sydney na Burj
Khalifa huko Dubai, pamoja na ishara muhimu ya mpira wa miguu wa China
unaenda ulimwenguni.
Timu ya Guangzhou Evergrande imekua ikicheza kwenye uwanja wa Tianhe wenye uwezo wa kubeba watazamaji 60,000 tangu 2011.
Kujenga
uwanja wenye uwezo wa kubebe watazamaji 100,000 imeelezwa kuwa inaweza
kuzidi uwezo wa siti 99,354 za kambi ya Barcelona Nou, ambapo kwa sasa
ndio uwanja mkubwa wa soka ulimwenguni.
Vilevile
imeelezwa kuwa ubunifu wa uwanja huo ni kazi kutoka kwa mbunifu kutoka
wa Amerika Hasan Syed, kufuatia wazo la awali kutoka kwa mwenyekiti wa
kikundi cha Evergrande Xu Jiayin huku kubuni umbo la ya maua ya lotus
inatokana hali ya Guangzhou kuwa jiji la Maua.
Uwanja
huo unajumuisha vyumba maalumu 16 vya (VVIP) vyumba vya kibinafsi vya
VIP (152) eneo la Shirikisho la Mpira Duniani (FIFA,) eneo la
wanariadha, eneo la vyombo vya habari, na chumba cha waandishi wa
habari.
Kwa mujibu wa
ESPN, Xia aliwaambia waandishi wa habari kwamba Evergrande ina mpango wa
kujenga kati ya viwanja vitatu hadi vitano vyenye uwezo wa kubeba
watazamaji 80,000 hadi 100,000 ikiwa ni sehemu ya kuwa mwenyeji wa
kombe la dunia kwa siku za baadaye.
Guangzhou Evergrande ni moja ya timu zilizofanikiwa zaidi nchini China na katika bara la Asia.
Klabu
hiyo imeshinda Ligi ya China Super mara nane, na pia Ligi mbili za
Mabingwa barani Asia ikiwa ni Klabu ya pekee ya China kushinda mara
mbili.
Msimu wa soka
(CS20) wa 2020 ulikuwa umepangwa kuanza mnamo Februari 22 uliahirishwa
kwa sababu ya janga la coronavirus ambapo China ilikua nchi ya kwanza
kuripoti janga hilo mwishoni mwaka jana.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...