Na Mwandishi wetu Mihambwe
Afisa
Tarafa Mihambwe amepinga vikali tabia mbaya ya kunyanyapaa Watu
wanaokuja toka kwenye maeneo ya wilaya na mikoa mingine kwa kuwahisi
wameambukizwa virusi vya Corona pasipo kuthibitishwa na Wataalamu wa
afya.
Gavana Shilatu
amewasisitiza Wananchi wa Tarafa ya Mihambwe kuzijua vyema dalili za Mtu
mwenye virusi vya Corona kama vile kikohozi kibichi, homa, maumivu ya
mwili, kuuma kwa koo na awe amethibitishwa na Wataalamu wa afya na sio
kuanza ubaguzi wa kunyanyapaana kama njia za kujikinga.
Gavana
Shilatu aliwaeleza njia za kujikinga ni kuosha mikono kwa sabuni kwa
maji yanayotiririka, kuepuka kugusana, kuepukana mikusanyiko, kuvaa
barakoa na si kunyanyapaana.
"Kuchukua
tahadhari haimaanishi kuanza dhambi ya ubaguzi ya kunyanyapaana kwa
kigezo cha Mtu kutoka kwenye maeneo tofauti, hii si sawa. Nakemea vikali
tabia hii, muhimu kujua dalili za ugonjwa wa Covid 19 ambazo mnazijua
na tuchukue tahadhari ya kujikinga na virusi vya Corona. Hakuna
tahadhali ya kujikinga inayosema tuwanyanyapae Watu, tuache tabia hii."
alisisitiza Gavana Shilatu.
Gavana
Shilatu alipita na timu ya Wataalamu wa afya na kutoa elimu ugonjwa wa
Covid 19 kwa njia ya matangazo na kuongea na Watu wanaokutana nao njiani
kwenye maeneo mbalimbali ndani ya Tarafa ya Mihambwe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...