Na Amiri kilagalila, Njombe

Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Njombe ikiongozwa na mwenyekiti
wa kamati hiyo ambaye ni mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri
imelazimika kufanya kikao chake cha kawaida nje ya ofisi wakiwa
wamesimama kwa kupeana nafasi takribani masaa mawili ili kutekeleza
agizo la kuto kukaa kwa karibu kwa lengo la kuzuia maambukizi ya
virusi vya CORONA (COVID-19).

Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri amewatoa hofu wajumbe wa kikao
hicho kutokana na mkao huo kwa kuwa ni utaratibu wa kawaida
uliofanyika ili kuepuka maambukizi ya Corona.

“Huu mkao wetu wa leo msiushangae,tumekaa hivi ni katika utekelezaji
wa maagizo ya kwamba tusikae kwa karibu hatukuona kama ni jambo jema
kukaa katika chumba tumejifungia,kwa hiyo hiki ni kikao chetu
rasmi”alisema Ruth Msafiri

Vile vile mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri amesema wameamua
kukutana ili kujadili mambo mbali mbali yanayohusu namna ya kudhibiti
maambukizi ya virusi vya Corona ,pamoja na kupokea taarifa rasmi
kutoka kwa kamati za afya za msingi za kila halmashauri zilizoundwa
ili kupambana na COVID-19.

“Kwa hiyo kutoka ofisi ya mkuu wa wilaya tuliunda kamati nne,ambazo
zinaigawa wilaya yetu katika tarafa nne kulingana na jumla ya tarafa
tulizonazo,kwa maana hiyo tumeona leo tupokea taarifa rasmi kuona nini
kimefanyika tangu tulipokutana pamoja na maendeleo yetu katika
udhibiti huu”alisema tena Ruth Msafiri

Waganga wakuu wa halmashauri za mji wa Njombe,Njombe dc na mji wa
Makambako dokta Isaya Mwasubila, dokta Deusdedit Kalaso na dokta
Alexender Mchome wakati wakitoa taarifa ya utekelezaji,wamesema
wanaendelea na uhamasishaji na utoaji elimu juu ya ugonjwa wa corona
kila pahala ndani ya maeneo yao ikiwa ni pamoja na kutenga maeneo
maalumu ya kuwahifadhia washukiwa wote endapo watapatikana.

“Sisi kama halmashauri ya mji wa Njombe tumefanya yafuatayo,tumetoa
elimu kwa watoa huduma wa vituo vya afya,hospitali na zahanati kwa
kuwa wao ndio wanaowapokea wagonjwa,lakini pia tumetoa elimu kwa jamii
namna ya kunawa mikono na namna ya kutumia vitakasa mikono,lakini pia
tumetenga kituo kwa ajili ya eneo la matibabu na wahisiwa watatengwa
pale hospitali ya mji kibena na sampo ikitoka wanakolona watahamishwa
kwenda kituo ambacho kipo km 50 kutoka makao makuu ya halmashauri ya
mji ambacho kinaitwa kituo cha afya Ihalula”alisema Yesaya Mwasubila
mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Njombe

Mkoa wa Njombe bado hakujaripotiwa kisa chochote cha mgonjwa wa
COVID-19 lakini mpaka sasa ripoti ya wizara ya afya nchini Tanzania
imethibitisha kuwapo kwa wagonjwa 20 hadi sasa katika mikoa ya dar es
salaam,kagera,arusha na visiwani Zanzibar huku wagonjwa wawili wakiwa
wamepona na mmoja kupoteza maisha.

 Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama katika kikao kilichofanyika nje ya ofisi namna halmashauri hiyo ilivyojipanga katika mapambano dhidi ya CORONA.
 Katibu tawala wa wilaya ya Njombe Emmanuel George pamoja na wajumbe wengine wa kikao cha kamati ya ulinzi na usalama kilichofanyika leo nje ya ofisi,wakiendelea kusikiliza taarifa za wajumbe namna walivyojipanga na mapambo dhidi ya COVID-19
 Wa kwanza kutoka kushoto ni dokta Deusdedit Kalaso mganga mkuu wa wilaya ya Njombe na wa pili ni dokta Isaya Mwasubila mganga mkuu halmashauri ya mji wa Njombe wakiwa makini kusikiliza taarifa za wajumbe juu ya mapambano ya CORONA.
Wajumbe wengine wa kamati ya ulinzi na usalama wakiendelea
kusikiliza taarifa za wajumbe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...