Na Anthony Ishengoma- Shinyanga

Athari za mlipuko wa ugonjwa wa Corona maalufu Covid 19 tayari
zimeanza kuonekana kutokana na wanunuzi wa madini ya Almasi kutoka
vikundi vya wachimbaji wadogo vinavyoendelea na marudio ya makinikia
ya mchanga wa almasi kuanza kupungua kwa kasi na wachimbaji hao
kushindwa kuuza madini hayo kwa wakati kama ilivyotarajiwa.

Hayo yamesemwa jana na Katibu Mkuu wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Shinyanga SHIREMA Bw. Gregory Kibusi wakati akiongea na vyombo vya habari kuhusu maendeleo ya zoezi la uchenjuaji wa makinikia ya almasi linaloendelea katika Kijiji cha Msagala Kata ya Maganzo Wilayani
Kishapu nje kidogo ya Mgodi Mkubwa wa Almasi wa Mwadui.

Bw. Kibusi aliongeza kuwa kupungua kwa wanunuzi wa madini hayo
kunatokana na wanunuzi wa almasi ndogo ndogo yenye ukubwa wa punje ya
sukari kupatikana Nchini India lakini kutokana na Nchi hiyo kukumbwa
na ugonjwa wa corona wahindi hawaji tena kununua madini hayo.

Kuhusu malalamiko ya wachimbaji wadogo hao kuhusu ubora wa mchanga huo
Bw. Kibusi amesema upatikanaji wa mchanga huo ambao ni takribani tani
milioni moja utaendelea kutolewa na mgodi wa Mwadui kwa kuwashirikisha
viongozi wa SHIREMA na kuwataka wachimbaji hao kuwa na subira na
tayari wamebadilisha mchanga huo baada ya mchanga wa awali kumalizika.

Bw. Kibusi aliongeza kuwa pamoja na changamoto zilizopo tayari makundi
sita yanayoundwa na vikundi miamoja tayari yanaendelea na uchenjuaji
wa makinia na yanaendelea kupata almasi ndogo ndogo na tayari
wamekusanya vipande vya almasi takribani 630 na kutokana na zoezi hilo
kuendelea wanatarajia kuendelea kupata vipande zaidi vya almasi.

Naye Afisa Madini Mkoa wa Shinyanga Bw. Bariki Munuo Afisa Madini Mkoa
wa Shinyanga aliongeza kuwa wachimbaji wanapata madini lakini
yanaifadhiwa na ofisi ya madini mkoa kutokana na madalali wa madini
kukosa mitaji jambo ambalo linachangiwa janga la corona.

Aidha Afisa huyo wa madini aliongeza kuwa kiwango cha madini hayo ni
kidogo kwa kuwa kikundi kinaweza kuchenjua kiwango kikubwa cha mchanga
na kupata kipande kidogo sana cha almasi na wakati mwingine kukosa
kabisa na changamoto nyingine wanapofanikiwa kupata mzigo unawekwa
ndani wasijue ni lini watafanikiwa kuuza kutokana na ufadhili wa watu
wanje kupunguza ufadhili kwa madalali wa madini.

Bw. Simon Malila ambaye ni mchenjuaji wa makinikia ya almasi
amepongeza mpango wa Serikali kufanikisha zoezi hilo lakini pia
hakusita kuomba kupatiwa mchanga unafaa zaidi na kudai kuwa mapato
yatakayopatikana kutokana zoezi hilo yatasaidia kuinua kipato cha
familia.

Pamoja na uwepo wa changamto ya kuporomoka kwa soko wachimbaji wadogo
katika vikundi vyao walionekana kutokata tamaa nakuendelea na zoezi
hilo na walipata moyo baada ya uongozi wa SHIREMA kufanikiwa
kuwabadilishia mchanga na mwandisahi wa habari hii alishuhudia makundi
hayo yakigombania mchanga mpya wenye mchanganyiko wa kokoto kubwa
ambao tofauti na awali ambapo wachenjuaji hao walitumia mchanga wenye
kiwango kidogo cha kokoto.

Ni Wiki sasa tangu vikundi vya wachimbaji wadogo wa madini ya almasi,
wilayani Kishapu, mkoani Shinyanga, vianze kunufaika na marudio ya
mchanga wa almasi kutoka mgodi Williamson Diamond limited, kufuatia
agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli
kuwaruhusu wachimbaji hao kunufaika na madini hayo.
 Baadhi ya vikundi vya wachimbaji wadogo wadogo wakiendelea na zoezi la uchenjuaji mchanga wa almasi kwa lengo la kutafuta almasi ndogondogo jana nje kidogo ya mgodi mkubwa wa almasi wa mwadui mkoani Shinyanga.
 Mchimbaji mdogo wa madini mkoani Shinyanga Makomba Faustine akiangalia kwa makini kama atafanikiwa kupata almasi wakati zoezi la uchenjuaji wa makinikia ya almasi linaoendelea nje kidogo ya mgodi mkubwa wa almasi wa mwadui mkoani Shinyanga.
Baadhi ya vikundi vya wachimbaji wadogo wadogo wakigombania mchanaga unaodhaniwa kuwa na vipande vya almasi wakati wa zoezi la uchenjuaji mchanga wa almasi kwa lengo la kutafuta almasi ndogondogo jana nje kidogo ya mgodi mkubwa wa almasi wa mwadui mkoani Shinyanga.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...