Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
JIWE
moja kubwa kati ya mawe makubwa yanayoelea nje ya uso wa dunia
(asteroid)ambalo limepewa jina la 52768 (1998 OR2) linategemewa kupita
pembeni ya dunia bila kuleta madhara yoyote hapo kesho Aprili 29, 2020,
Shirika la utangazaji CNN limeripoti.
Imeelezwa
kuwa tukio hilo linatagemewa kutoka kesho katika majira ya 4:56
alfajiri kwa mujibu wa Wakala wa vyombo vya anga za nchi za chini na
anga za mbali nchini Marekani (NASA.)
Licha
ya watu kuwa na sitofahamu kuhusiana na jiwe hilo na muelekeo wake wa
kulenga dunia mtaalamu kutoka NASA Steven Pravdo amesema, jiwe hilo
litapita kilomita milioni 6 kutoka duniani na halitakuwa na athari
yeyote.
Jiwe
hilo linakadiriwa kuwa na ukubwa kati ya kilomita 1.8 hadi 4.1 litapita
pembeni ya dunia kwa maili 3,908,792 ikitumia maili 29,461 kwa saa.
Imeelezwa kuwa jiwe hilo lililoanza kutua mwaka 1998 halitarajiwi kuleta athari yoyote.
Imeshauriwa
wenye darubini za kuangalia anga za mbali wanaweza kuliona jiwe hilo
likitembea anga za mbali taratibu mithili ya nyota katika tarehe tajwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...