Na Shukrani Kawogo

WAJUMBE wa Kamati ya Wataalamu tisa  iliyoundwa na mawaziri wanne kutoka  Wizara mbalimbali ili kumsaidia mzee Reuben Mtitu (Mzee Kisangani) kuweza kupanua kiwanda chake kwa kupata malighafi, eneo kubwa, pamoja na vitu muhimu ambavyo vitamsaidia kukuza kiwanda hicho imewasili wilayani Ludewa mkoani Njombe ambapo itafanya kazi hiyo kwa muda wa siku 15.

Kamati hiyo iliundwa Machi 30 mwaka huu na Waziri wa Madini Dotto Biteko, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mussa Zungu, Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) Mwita Waitara pamoja na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya,

Pia kikao hicho kilihudhuriwa na watu kutoka katika Shirika la Mendeleo la Taifa (NDC), Baraza la Taifa la Kuhifadhi Mazingira (NEMC) na wataalamu kutoka Wizara ya Madini pamoja na Tume ya Madini.

Kamati hiyo iliongozwa na Mwenyekiti wao Sylivester Mpanduji (SIDO) pamoja na wajumbe wengine Wilfred Machumu kutoka Tume ya Madini, Issa Mtuwa kutoka Wizara ya Madini, Abbas Mruma (GST), Prof. Madundo Mtambo(TIRDO), Dr. Yohana Mtoni (NDC), Anorld Mapinduzi (NEMC), Leo Mavuka (TAMISEMI) pamoja na Dr. Hellen kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe, imewasili na kuanza kazi ya kutafiti maeneo mbalimbali ambapo ilianzia eneo la Mchuchuma ambako kuna makaa ya mawe pamoja na madini mbalimbali.

Ikumbukwe kuwa uundwaji wa kamati hii ni matokeo ya ziara ya waziri wa madini Dotto Biteko alipotembelea katika kiwanda kidogo cha mzee huyo ambaye anatengeza zana mbalimbali za chuma ambapo mzee huyo alitoa chngamoto zake ikiwemo ukosefu wa makaa ya mawe ambapo Biteko aliahidi kukaa na viongozi wenzake ili kumsaidia.

Biteko amesema sera ya serikali hii ni ya viwanda hivyo hana budi kuinua watu wanaothubutu kuanzisha viwanda hivyo kama ambavyo alivothubutu mzee Reuben katika kuanzisha utengenezaji wa zana hizo yakiwemo mapanga, shoka na nyundo tena yenye uubora wa hali ya juu.
Sehemu ya  Mto mchuchuma ambao umetawaliwa na makaa ya mawe
Moja ya eneo la uchimbaji wa makaa ya mawe lilipo mchuchuma.
 Timu ya wataalamu ikiangalia mtambo (kinu) cha kuyeyushia madini
 Wanakamati wakiangalia moja ya eneo la uchimbaji makaa ya mawe katika eneo la mchuchuma lililopo kata ya Mkomang'ombe wilayani Ludewa Mkoani Njombe

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...