Na Karama Kenyunko Michuzi TV.
KESI ya kughushi Cheti Cha ndoa inayomkabili aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Ilala, Norah Waziri maarufu kama Nora Mzeru itaanza kuunguruma katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni Juni 2, mwaka huu.
Hatua hiyo imekuja baada ya wakili wa serikali Mkuu, Yussuf Aboud kudai mbele ya Hakimu Mkazi mfawidhi, Frank Moshi wa mahakama hiyo kuwa, kesi hiyo leo ilipangwa kwa ajili ya kuanza kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka lakini hawakuwa na mashahidi.
Kufuatia taarifa hiyo mahakama imeahirisha kesi hiyo mpaka Juni 2,mwaka huu ambapo mashahidi watatu wa upande wa mashtaka wanatarajia kuanza kutoa ushahidiwao siku Hiyo.
Wakati kesi hiyo ikiahirishwa Mshtakiwa Nora alikuwepo mahakamani hapo
Katika Kesi ya msingi Nora anadaiwa kuwa Februari 4,1995 jijini Dar, es Salaam, kwa nia ya kudanganya, alighushi cheti cha ndoa chenye usajili namba 00040078 kwa nia ya kuonesha kuwa alifunga ndoa na marehemu Silvanus Mzeru Februari 4, 1995 katika kanisa la Roman Catholic la Mburahati wakati wakijua si kweli.
Katika shtaka la pili Nora anadaiwa kutumia cheti hicho cha ndoa cha kughushi kuomba usimamizi wa mirathi katika Mahakama Kuu ya Dodoma.
Hata hivyo, mshtakiwa huyo yupo nje kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya dhamana yaliyomtaka kuwa na wadhamini wawili ambapo mmoja kati ya wadhamini hao atoke katika Taasisi inayotambulika kisheria.
Mbali na masharti hayo kila mdhamini alisaini bondi ya Sh 1milioni .

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...