NA MWAMVUA MWINYI, CHALINZE
MAFUNDI
binafsi wa ujenzi katika Kitongoji cha Mbukwa Kijiji cha Lugoba, Kata
ya Lugoba na Kijiji cha Mbwewe Kata ya Mbwewe Chalinze ,Bagamoyo Pwani,
wamesema serikali imewapatia fursa ya ujenzi wa miradi mbalimbali,hali
inayowasaidia kujiongezea kipato.
Wakizungumza
katika Kitongoji cha Mbukwa na Changarika wilayani hapo, mafundi Rajabu
Mdoe na Haruni Mohamed walisema ,hatua hiyo imewapatia pia nafasi ya
kuonyesha uwezo na ujuzi wao katika kujenga vyoo na vyumba vya madarasa.
"Serikali
ya awamu ya tano inatekeleza mengi na kutetea wananchi wanyonge ,na kwa
hili sisi kupewa nafasi kuinua maisha yetu inatusaidia na familia
zetu,"
Mdoe anayejenga
matundu ya vyoo shule ya Sekondari Changarikwa alieleza kuwa, licha ya
hayo, mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha kuchelewesha kufika
vifaa vinavyotumika kwa ujenzi, lakini wanatarajia kukamilisha kwa
wakati.
Nae Haruni
alieleza,anajenga vyumba viwili vya madarasa katika shule mpya ya
Mbukwa, na kwamba mbali ya vyumba hivyo tayari ameshakabidhi chumba
kimoja alichokikamisha miezi michache iliyopita.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...