Meya wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam
Alhaj Abdallah Chaurembo (wa pili kulia)akipokea msaada wa barakoa, glovu
pamoja na Sanitizer kutoka kwa Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya General Petroleum Ltd Hayatulah Khan(wa tatu
kushoto) kwa ajili ya kugawa kwa watumishi na watendaji wa manispaa hiyo.Msaada
huo umekabidhiwa leo ikiwa ni mkakati wa kampuni hiyo kuunga mkono jitihada
za Serikali ya Awamu ya Tano katika kukabiliana na ugonjwa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya General
Petroleum Ltd Hayatulah Khan(aliyesimama) akizungumza mbele ya watendaji na
watumishi wa manispaa ya Temeke jijiini Dar es Salaam kabla ya kukabidhi msaada
wa Sanitizer, Barakoa pamoja na glovu ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na
ugonjwa wa Covid-19.Aliyekaa ni Meya wa Manispaa ya Temeke Alhaj Abdallah
Chaurembo
Meya wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam
Alhaj Abdallah Chaurembo akizungumza leo kwenye ukumbi wa manispaa hiyo kabla
ya kupokea msaada wa barakoa, sanitizer na glovu kutoka Kampuni ya General Petroleum(GP) kwa ajili ya
kukabiliana na ugonjwa Covid-19.
Viongozi wa ngazi mbalimbali wa Manispaa ya
Temeke jijini Dar es Salaama wakiwa ukumbini wakati wa upokeaji wa msaada wa
vifaa vya Barakoa, Sanitizer na Glovu ambazo zimetolewa na Kampuni ya General Petroleum.
Meya wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam
Alhaj Abdallah Chaurembo(kushoto) akiteta jambo na Mganga Mkuu wa Manispaa hiyo
Gwamaka Mwabulambo(kulia) baada ya kupokea msaada wa Sanitizer, Barakoa na
Glovu ambazo ni msaada kutoka Kampuni ya General Petroleum kwa ajili ya
kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19 unaosabishwa na virusi vya Corona.
Baadhi ya maofisa kutoka Kampuni ya General
Petroleum wakiwa pamoja na Meya wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam(wa
kwanza kulia), wakiwa na Sanitizer kabla ya kuanza kwa kugawa kwa watendaji ,
madiwani na watumishi wa manispaa hiyo.
Sehemu ya maofisa wa Kampuni ya General
Petroleum (waliovaa fulana) wakiwa katika ukumbi wa Manispaa ya Temeke jijini
Dar es Salaam .Wengine ni viongozi wa manispaa ya Temeke wakifuatilia maelekezo
ya kutumia vifaa vilivyotolewa kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa virusi vya
Corona.
Baadhi ya madaktari na wauguzi wa Hospitali ya T
emeke jijini Dar es Salaam wakipaka Sanitizer baada ya kupewa msaada huo kutoka
Kampuni General Petroleum.
Meya wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam
Alhaj Abdallah Chaurembo(kulia) akikabidhi Sanitizer kwa Mganga Mkuu wa
Hospitali ya Mbagala leo.Msaada huo umetolewa na Kampuni ya General Petroleum.
Meya wa Manispaa ya Temeke Alhaj Abdallah
Chaurembo(kulia) akikabidhi kasha lenye Sanitizer kwa Ofisa Ugawi katika
Hospitali ya Temeke Khalid Mtaraziki.Wengine ni maofisa wa Kampuni ya General
Petroleum.
Diwani wa Kata ya Kilungule Said Fella akiwa na
baadhi ya viongozi wa manispaa ya Temeke wakati wa utolewaji wa msaada wa
Sanitizer, glovu na barakoa.
Na Said Mwishehe, Michuzi TV
KAMPUNI ya General Petroleum imekabidhi msaada
wa Sanitizer, barakoa na glovu kwa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar
es Salaam ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika mapambano dhidi ya virusi
vya Corona huku Meya wa Manispaa hiyo Alhaj Abdallah Chaurembo akisisitiza
umuhimu wa wananchi kufuata maelekezo ya watalaam wa afya.
Akizungumza leo wakati wa kupokea vifaa hivyo Meya Chaurembo amesema
Wilaya ya Temeke imekuwa ikichukua tahadhari katika kukabiliana na ugonjwa huo
kwa kuwakumbusha wananchi kuendelea kufuata maelekezo ya watalaam wa afya na
kwamba msaada ambao wameupata kutoka kwenye kampuni hiyo umekuja wakati muafaka
na kwamba watahakikisha unawafikia wananchi mbali ya viogozi na watendaji.
"Vifaa hivi vitasabazwa kwenye Kata zote za Manispaa hii,
niwaombe wananchi kuvitumia kwa kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalam wa afya,
lakini pia tuendelee kuchukua tahadhari kama ambavyo Serikali
inatuelekeza," amesema Alhaj Chaurembo.
Aidha,amesema vifaa hivyo vitapelekwa pia kwenye hospital ya
rufaa ya Mkoa ya Temeke pamoja na Hospital ya Wilaya ya Mbagala Zakheem.Ambapo baada ya kutoka katika manispaa hiyo walikwenda
kukabidhi msaada huo kwa hospitali hizo.Pia amekabidhi kwa watendaji na
madiwani wa kata zote zilizopo ndani ya manispaa hiyo.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dk. Gwamaka
Mwabulambo amesema wananchi wanatakiwa kufahamu kuwa ugonjwa huo hauna tiba na
jambo muhimu ni kuchukua tahadhari."Tuendelee kuchukua tahadhari Kwa
kuepuka msongamano na kushikana mikono."
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Hayatulah
Khan amesema baada ya kuona jitihada ambazo zinafanywa na Serikali
katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo , wameona wanayo nafasi ya wao kusaidia
vifaa vya kukabiliana na Corona na hivyo wamekabidhi msaada wao kwa manispaa ya
Temeke."Tupo tayari kuendelea kutoa msaada zaidi katika kukabiliana na
ugonjwa wa Covid-19."
Wakati huo huo Ofisa Rasilimali watu wa General Petroleum,
Aboubakar Kondo, amefafanua kampuni yao inaguswa na tatizo lililoikumba
Tanzania na Dunia kwa ujumla la virusi vya Corona,hivyo wameona ni vema wakasaidia vifaa hivyo kwa
kupeleka manispaa ya Temeke, Hospitali ya Mkoa wa Temeke pamoja na Hospitali ya
Mbagala na kwamba wataendelea kugawa na kwa wananchi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...