Jaji Kiongozi Dkt. Feleshi (wa pili kushoto) akisalimiana na watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Pwani. Mhe. Jaji. Dkt. Feleshi amewataka Mahakimu na Watumishi wa Mahakama kwa ujumla kuongeza kasi ya usikilizaji wa mashauri ikiwa ni moja ya mbinu ya kukabiliana na ugonjwa hatari wa 'corona' unaoikabili dunia.
Jaji Kiongozi Dkt. Feleshi akizungumza na mmoja wa Wazee wa Baraza (Wa kwanza kushoto) wa Mahakama ya Mwanzo Mailimoja.
Jaji Kiongozi Dkt. Feleshi akijadiliana jambo wakati wa ukaguzi Mahakama ya Mwanzo Msoga. Wa pili kushoto ni Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Pwani, Bw. Moses Minga.
Jaji Kiongozi Dkt. Feleshi akizungumza na Mahakimu na Watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Mwambao.
Jaji Kiongozi Dkt Feleshi (kushoto) akiongea na washitakiwa (waliokaa) katika Mahakama ya Mwanzo Mwambao.
Jaji Kiongozi Dkt Feleshi akisalimiana na watumishi wa Mahakama ya Wilaya Bagamoyo.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Bagamoyo, Mhe. Munga Sabuni (aliesimama) akiwasilisha taarifa ya Mahakama hiyo kwa Jaji Kiongozi.
Jaji Kiongozi Mahakama Kuu ya Tanzania Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi (kulia) akisalimiana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Pwani, Mhe. Joyce Mkhoi (kushoto) alipowasili mjini Kibaha, April 1, 2020 tayari kwa kuanza ziara ya ukaguzi Mkoani Pwani.
Jaji Kiongozi, Dkt Feleshi na Maafisa wa Mahakama alioambatana nao wakinawa mikono kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa ‘corona’ kabla ya kuingia ndani ya jengo la Mahakama ya Hakimu Mkazi , Pwani.
(Picha na Rashid Omar, Mahakama ya Hakimu Mkazi-Pwani)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...