Na Leandra Gabriel, Michuzi Media TV
LEO
Aprili 2 dunia inaadhimisha siku ya kimataifa ya kuhakikisha ukweli wa
taarifa juu ya mambo yanayosikika ( World Fact Checking Day) ni siku ya
kila mmoja kutafakari juu ya taarifa kuhusu taarifa anayopokea na
kuipeleka kwa watu wengine.
Ikiwa
ni maadhimisho ya tatu kufanyika mtandao wa uhakiki wa taarifa duniani
(IFNC) umeeleza kuwa maadhimisho ya siku hiyo ni kwa kila mmoja wakiwemo
wananchi, wanahabari na wataalamu wa uhakiki wa taarifa ikiwa ni katika
kuzuia na kupambana na usambaaji wa taarifa zisizo na ukweli.
Katika
maadhimisho hayo kwa mwaka huu wananchi kote duniani wameshauriwa
kusambaza taarifa za kweli zilizothibitishwa na kutolewa na mamlaka
husika katika wakati huu ambao dunia inapambana na janga la virusi vya
Covid 19.
Imeelezwa kuwa ni wajibu wa kila
mmoja kupunguza na kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo na hiyo ni pamoja na
kufahamu vyanzo vya kuaminika vya taarifa ni hatua muhimu kabisa.
Wataalamu
kutoka mtandao wa uhakiki wa taarifa duniani (IFNC) wamewashauri
wananchi kote duniani kutumia mitandao ya kijamii vyema kwa kutoa
taarifa za kuelimisha zaidi jamii kuhusiana na mlipuko wa virusi vya
Corona.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...