Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

MRATIBU  wa Shirika lisilo la kiserikali la Utepe Mweupe (White Ribbon), nchini  Rose Mlay ameiomba serikali kuongeza idadi ya wakunga katika vituo vya afya, zahanati na hospitali za mikoa ili akina mama wapate huduma nzuri pindi wanapojifungua.

Akizungumza na Michuzi Tv  wa kuelekea Kampeni ya "Wanawake wanataka nini ,Sikiliza Chukua Hatua" iliyoandaliwa na Shirika hilo amesema katika uzazi kuna chabgamoto nyingi wakati wa kujifingua hivyo wanaiomba serikali kuwekeza wakunga na wauguzi wenye ujuzi .

Mratibu huyo amesema wanatamani  kuona hospitali za Wilaya ziwe na wakunga 20, hospitali ya Rufaa na Mkoa wawe 102 wanaofanya kazi za ukunga tu lengo ni kuwaangalia akina mama wanaenda kujifingua kwa ukaribu zaidi.

"Tunaomba wizara ya afya iongeze wakunga wa katika kila kituo cha afya angalau wawe wakunga watano wanaofanya kazi ya ukunga tu kwani kwa sasa ukienda utakuta mkunga mmoja au wawili ambapo idadi ndogo ikilinganishwa na akina mama wanaojifungua kwa siku," ameeleza Rose.

Rose aneongeza kuwa utafiti walioufanya katika Mikoa 10 kwa kuwauliza wanawake 110,000 alisilimia 8.61 ya wanawake hao walitaka huduma za uzazi zenye heshima na utu.

Amesema  asilimia 8.99 walitaka madawa na vifaa ,asilimia 7.56 walitaka huduma zilizoboreshwa na ustawi na afya ya uzazi kwa ujumla,asilimia 7.32 na pia walitaka kuongezwa vituo vya afya vyenye ukamilifu na kwamba wengine  waliotaka ushauri nasaha, ufahamu kuhusua afya ya uzazi walikuwa 7.17.
 Mratibu wa Utepe Mweupe Rose Mlay akizungumza kuhusiana na Kampeni ya Wanawake Wanataka Nini katika huduma za Uzazi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...