Na Ahmed Mahmoud Arusha.
SHIRIKA la
Mtandao wa Wafugaji na Wawindaji sanjari na Waokota Matunda la PINGO'S
limetoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya milioni 18.2
kuisaida Serikali kwenye mapambano ya Ugonjwa wa Covid 19.
Vifaa
hivyo vilikabidhiwa kwa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro kwa niaba ya
jamii ya Wafugaji wilayani humo kwaniaba yao kwa Mkurugenzi wa
halmashauri hiyo Yafred Myenzi
Akiongea
wakati akikabidhi vifaa hivyo Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya Pingo's
Edward Parokwa alisema kuwa wilaya hiyo imepakana na mikoa mitatu hivyo
muingiliano huo unaifanya wilaya hiyo kuweza kupata kwa urahisi Ugonjwa
huo.
Alisema jamii hiyo
imekuwa ikiuza dawa za kienyeji maeneo mengi nchini na hata nje ya nchi
hivyo uwezekano wa kuja na maambukizi ndio umepelekea wao kuanza nao
kuwapatia vifaa vya kujikinga na Ugonjwa huo wa Covid 19.
Akabainisha
idadi ya vifaa walivyokabidhi na lengo la kusaidia wilaya hiyo kuwa
inamuingiliano wa wageni wanaotoka nchi jirani kufika kununua mifugo pia
inapakana na mikoa minne ya Dodoma,Arusha,Kilimanjaro na Tanga kwa kuwa
vijana wengi wanauza madawa maeneo mengi Kuna uwezekano wa kuja na
magonjwa ya Covid 19.
"Jambo
lililotufanya tuone umuhimu wa kupeleka vifaa hivi kwenye wilaya hii ni
kutokana na muingiliano wa vijana wetu wengi wanafanya biashara ya
kuuza dawa za kienyeji maeneo mengi nchini na nje ya nchi hivyo
uwezekano wa kuja na maambukizi ni mkubwa"
Kwa
Upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt.Elizabeth Oning'o alisema
kuwa vifaa hivyo vimekuja wakati muafaka na vitasaidia mapambano ya
kukabiliana na Ugonjwa wa Covid 19 wilayani humo.
Alisema
wilaya hiyo imekuwa na uhitaji mkubwa wa vifaa hivyo kutokana na kuwa
na migodi ya Tanzanite Jambo linalohitaji vifaa vya kujikinga na kwa
Sasa vitasaidia kwa kuwa walikuwa na upungufu kwenye kambi zao na vituo
vyao vya Afya wilayani humo.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Yafred
Myenzi amelipongeza shirika hilo la Pingo's Forum kwa kuamua kusaidia
wilaya hiyo kwenye mapambano ya janga la Ugonjwa wa Covid 19.
Alisema
kuwa wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa ya mwingiliano
kutokana na wakazi wengi wanafanya shughuli zao nje ya wilaya hali
inayotishia uwezekano wa kuwa na wagonjwa wengi.
Mkurugenzi
wa Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro Yafred Myezi akipokea
vifaa vya mapambano ya Ugonjwa wa Covid 19 kutoka kwa Mkurugenzi wa
Pingo's Forum Edward Porokwa Kwenye makao makuu ya shirika hilo Sakina
Jijini Arusha picha na Ahmed Mahmoud Arusha.
Pichani ni sehemu ya vifaa vilivyotolewa na shirika la Pingo's Forum
kwa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro kwa ajili ya mapambano ya Ugonjwa
wa Covid 19 vinavyosababishwa na virusi vya korona vyenye thamani ya
milion 18.2 picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...