Benki Kuu ya Tanzania (BOT) inapenda kuutarifu
umma kuwa, kufuatia maelekezo ya Serikali kutaka wananchi kuchukua tahadhari za
kujikinga na ugonjwa wa Covid-19 unaosababishwa na virusi vya Corona, kuanzia siku ya Jumatano tarehe 22 Aprili
2020, wananchi wote watakaotembelea ofisi za Benki Kuu kote nchini watatakiwa kuvaa barakoa (masks)
kwa lengo la kujikinga wao wenyewe na kuwakinga wafanyakazi watakaowahudumia
dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.
Katika kuepuka msongamano, Benki Kuu inawaomba
wateja wake na wananchi kwa ujumla pale inapowezekana, watumie njia mbadala za
mawasiliano badala ya kwenda kwenye ofisi za Benki Kuu. Njia hizo ni pamoja na
kupiga simu, kutuma barua pepe kupitia info@bot.go.tz
au botcommunication@bot.go.tz na
pia kutumia nukushi (fax) namba +255 22 2234217. Aidha, wananchi wanaweza
kupata taarifa mbalimbali za Benki Kuu kupitia tovuti yake ya www.bot.go.tz.
Tunatoa wito kwa wananchi wote kuzingatia
maelekezo yanayotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto kuhusu namna ya kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya maambukizi ya
virusi vya Corona ikiwa ni pamoja na kunawa mikono na kutumia vitakasa mikono
(sanitizers) kila mara na kuepuka msongamano.
Benki Kuu itaendelea kutoa huduma kwa kuzingatia
tahadhari zote zinazotakiwa kuchukuliwa dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.
Namba
za Simu kwa Ofisi za Benki Kuu ya Tanzania
Na.
|
Ofisi
ya BOT
|
Namba
ya Simu
|
1.
|
Dar es Salaam (Makao Makuu)
|
+255 22 2234496/7
|
2.
|
Zanzibar
|
+255 24 2230803
|
3.
|
Arusha
|
+255 27 254 5541-3/ +255 27 254 5482
|
4.
|
Dodoma
|
+255 26 296 3183/7
+255 22 223 2506
|
5.
|
Mbeya
|
255 25 250 3321-3
|
6.
|
Mtwara
|
+255 22 223 2650-1
+255 22 223 2664
|
7.
|
Mwanza
|
+255 28 250 0313/17
|
8.
|
Chuo cha BOT Mwanza
|
+255 28 250 0709
+255 28 250 0983
|
Imetolewa na
Idara
ya Uhusiano na Itifaki
April 21, 2020
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...