MITANDAO
mingi ya kijamii ikiwemo Facebook, WhatsApp na TikTok, inaongelea
video zao... video za kundi linalofanya shughuli za mazishi kutoka nchini Ghana
linalojulikana kama Prampram Pallbearers ambalo kwa sasa limekua
maarufu zaidi ulimwenguni kote.
Video
la kundi hilo zinawaonesha wanaume watano waliovalia nguo nyeusi,
miwani nyeusi wakiwa wamebeba jeneza wakisindikizwa na kibao cha
"Astronomia" wimbo ulioimbwa na Tony Igy.
Mwanzilishi
wa kundi hilo Benjamin Aidoo akizungumza na "The Ghana report" ameeleza
kuwa, alianza biashara hiyo mwaka 2007 na umaarufu wao mpya unaweza
kushawishi kupandisha viwango vya huduma mara baada ya janga la Corona
(Covid -19) kumalizika.
"Umaarufu
ambao tunaupata sasa unakuza biashara yetu na tunaweza kuongeza gharama
baada ya kutoweka kwa mlipuko wa virusi vya Corona na kwa sasa tuna
msimamizi na wakili nchini Kenya" ameeleza.
Aidoo amesema kuwa lazima kuwa mbunifu zaidi ili kufanikisha jambo lako;
"
Hapa Ghana lazima uwe mbunifu, niligundua kuwa katika mazishi watu
wengi huvaa nguo nyeusi lakini nilitaka kwangu iwe tofauti kwa hiyo
nikaongeza rangi nyeupe, nyeusi na nyekundu" amesema.
Akifafanua
kiwango cha gharama za huduma zao Aidoo amesema, bei hutegemea na
mavazi waliyovaa na kusema kuwa mavazi meusi na meupe kwa kikundi hicho
katika shughuli za mazishi ni gharama za chini zaidi kwa kampuni hiyo.
Kuhusiana
na gharama za huduma hiyo Aidoo amesema kuwa kiwango cha juu zaidi ni
dola za kimarekani 3000 ukiondoa usafiri, chakula na malazi kwa shughuli
waliyoifanya nje ya nchi.
Pia ameeleza kuwa kundi hilo la mazishi litaendelea kuongeza vionjo ili kuweza kuendelea kuwa tofauti.
Akieleza uzoefu wa kazi hiyo, Aidoo amesema kuwa;
"Tulifanya
kazi kwa familia moja huko Kumasi mwaka jana, maiti ilikuwa nzito kiasi
kwamba hatukuweza kunyanyua kidole kwa wiki mbili baada ya hapo"
amesema Aidoo.
Kwa sasa
ambapo dunia inapambana na mlipuko wa homa ya mapafu inayosababishwa na
virusi vya Corona mabango makubwa yenye picha ya wanaume hao
yanaongezeka kote ulimwenguni ikiwa ni ishara ya kuwahimiza watu kukaa
nyumbani au kujiunga nao kama maiti kwenye sinema yao ya kurudi kwenye
kaburini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...