Na Ahmed Mahmoud Arusha

Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesitisha kwa muda kuendelea na shughuli yeyote kwenye eneo la Losirwa kata ya Moshono hadi Serikali itakapotoa maelekezo Mengine ambapo amewaonya Wenyeviti wa Mitaa kuacha kuchukuwa fedha na kutoa vibali vya Ununuzi wa Ardhi kwenye maeneo yenye Migogoro.

Aidha Amezitaka halmashauri za wilaya kuacha kutoa vibali vya ujenzi kwa wananchi kwenye maeneo yenye migogoro kwa kuwa inaleta mikanganyiko kwenye jamii na kuleta ugumu wakati wa kuitatua. Gambo ametoa kauli hiyo Jana wakati alipotembelea kuona eneo lenye mgogoro baina ya Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ) kikosi Cha 977 kj na wakazi wa eneo la Losirwa kata ya Moshono jijini Arusha uliodumu kwa muda mrefu Sasa.

Akiongea Mara baada ya kukagua eneo hilo na kusikiliza pande zote ametoa maagizo hayo na kueleza kuwa wananchi waendelee kuwa watulivu hadi Serikali itakapotoa maelekezo mapya kufuatia mgogoro huo. Alisema kuwa wananchi wengi wanajielewa kama Kuna mtu anaendelea na ujenzi aaxhie hapo hapo hadi Serikali itakapotoa maelekezo mapya.

“Tunaunda tume ya wataalamu kupitia upya na watatoa mapendekezo baada ya taarifa ndipo tutatoa maamuzi lakini kwa Sasa shughuli zote nimezisitisha” Alibainisha kuwa Wenyeviti na Tarafa na vijiji wanaopitishia watu vibali vya kununua Ardhi watawachukulia hatua za kisheria kwani wao ndio chanzo Cha kuwaingiza wananchi kwenye migogoro.

Kwa Upande wao wananchi wa eneo hilo Regina Elias na Poulo Mollel wakizungumza wameitaka Serikali kuangalia suala hilo kwa kina na kufanya Tathmini upya kwani wao wameishi muda mrefu eneo hilo na wanategemea maeneo hayo kwa kujipatia riziki zao za kila siku.

Walisema kuwa fedha walizopata kama fidia bado hazilingani na maeneo yao utakuta mtu amelipwa kiasi kidogo na mwingine amelipwa eneo kama hilo kiasi kikubwa kwa eneo lenye ukubwa kama huo na Tathmini imekaa muda wa miaka sita ndipo malipo yamekuja kulipwa bila maandishi yeyote hali inayoleta mkanganyiko kisheria. Moja ya wananchi akitoa maelezo mbele ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akieleza na kuomba Serikali kuangalia hatma yao kwani wao wanategemea eneo hilo kuendesha maisha yao kama walivyokutwa na kamera ya matukio jijini Arusha.

Sehemu ya makazi ya wananchi wa eneo la Loswira kata ya Moshono ambao Jana mkuu wa mkoa wa Arusha alipita kukagua mipaka yao na JWTZ kikosi Cha 977 kj kwenye mgogoro uliodumu kwa muda mrefu picha na Ahmed Mahmoud Arusha.
Picha ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akipata maelezo kutoka kwa viongozi wa JWTZ wakati walipofika kukagua mipaka ya eneo hilo ikiwa ni kujionea na mwisho kutoa maamuzi ya mgogoro huo. Moja ya nyumba za wakazi eneo la Losirwa kata ya Moshono kama zilivyokutwa na kamera ya matukio jijini Arusha picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...