Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi.
Zainabu Tellack akiongea na wafanyibiashara wa mnada wa mifugo wa
Muhunze ulioko Wilayani Kishapu jana alipofika katika mnada huo kujionea
namna bora ya uzingatiaji wa maelekezo ya Serikali kuhusu kujikinga na
mlipuko wa ugonjwa wa Corona.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi.
Zainabu Tellack akiongea na wafanyibiashara ndogo ndogo wa matunda na
nyanya kando ya mnada wa mifugo wa Muhunze ulioko Wilayani Kishapu
jana alipofika katika mnada huo kujionea namna bora ya uzingatiaji wa
maelekezo ya Serikali kuhusu kujikinga na mlipuko wa ugonjwa wa Corona.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi.
Zainabu Tellack akionesha mfano wa namna bora ya kunawa wa Mikono kabla
ya kuanza ukaguzi wa Kituo cha Afya Kishapu kitachotumika kuhudumia
wagonjwa Corana kama atatokea mgonjwa wa ugonjwa huo Wilayani Kishapu
jana alipofika katika kituo hicho kujionea namna bora ya uzingatiaji wa
maelekezo ya Serikali kuhusu kujikinga na mlipuko wa ugonjwa wa Corona.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi.
Zainabu Tellack akionesha mfano wa namna bora ya kunawa wa Mikono kabla
ya kuanza ukaguzi wa Kituo cha Afya Kishapu kitachotumika kuhudumia
wagonjwa Corana kama atatokea mgonjwa wa ugonjwa huo Wilayani Kishapu
jana alipofika katika kituo hicho kujionea namna bora ya uzingatiaji wa
maelekezo ya Serikali kuhusu kujikinga na mlipuko wa ugonjwa wa Corona.

Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga Bi. Zainabu Tellack akiongea na wafanyibiashara ndogo ndogo wa
matunda na nyanya kando ya mnada wa mifugo wa Muhunze ulioko Wilayani
Kishapu jana alipofika katika mnada huo kujionea namna bora ya
uzingatiaji wa maelekezo ya Serikali kuhusu kujikinga na mlipuko wa
ugonjwa wa Corona.
…………………………………………………………………………………
Na Anthony Ishengoma- Sinyanga
Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga Bi. Zainabu Tellack amewataka wazazi na walezi mkoani
Shinyanga kutowaruhusu watoto wadogo kwenda katika mikusanyiko hususani
minada ya mazao na mifugo kama hatua muhimu ya kuwakinga na maambukizi
ya ugonjwa wa corona.
Mkuu wa Mkoa
ameyasema hayo wakati alipotembelea mnada wa mifugo wa Muhunze ulioko
katika Makao Makuu ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga kwa lengo la
kujionea utekelezaji wa agizo la serikali linalowataka wananchi kuchukua
tahadhari ya kujikinga na ugonjwa wa corona ikiwemo kuweka maji na
sabuni katika maeneo yanayokutanisha watu wengi pamoja na kukaa umbali
wa mita moja.
Bi. Tellack
ameonya kuwa huu si wakati wazazi kutembea na watoto wao kutokana na
uwepo wa mlipuko wa ugonjwa wa Corona na kuwataka kusubiri mpaka wakati
ugonjwa huu utakapokuwa umedhibitiwa kwani uwezo wa watoto kujikinga ni
mdogo sana.
Pamoja na agizo
hilo la Mkuu wa Mkoa kwa wakazi na wafanyabiashara katika minada ya
mifugo pia hakuridhishwa na hatua za zuinazochukuliwa na uongozi wa
mnada huo za kuhakikisha wale wote wanaoingia mnadani hapo wanasafisha
mikono yao baada ya kujionea mnada huo ukiwa na njia zaidi ya moja ya
kuingia mnadani hapo na kutoa nafasi kwa baadhi ya watu kujipenyeza
ndani ya eneo hilo bila kuchukua tahadhari ya kujikinga na Corona.
Bi. Tellack
amewataka wafanyabiashara mnadani hapo kuhakikisha wanajikinga na
maambukizi hayo kwa kila mmoja kunawa mikono yake kila mara na
kuhakikisha wanakuwa na vitakasa mikono (sanitizers) kwa vile wanao
uwezo wa kuvinunua kama hatua muhimu ya kujikinga na hatari ya
maambukizi hayo.
‘’Nunueni
vitakasa mikono kwa ajili ya usalama wenu kwa sababu hamuwezi kukosa
fedha ya kununua ya kiasi cha shilingo elfu nne na miatano na hata kama
ni shilingi elfu kumi kwa ajili ya kujikinga na kuwakinga
wengine.’’Aliendelea kusema kiongozi huyo wa Mkoa.
Agizo kama hili
pia lilitolewa na Mkuu wa Mkoa kwa wafanyabiashara ndogo wanaofika eneo
la mnada kwa lengo la kujipatia kipato tofauti na mifugo inayouzwa
mnadani kuhakikisha wanakuwa na maji na sabuni vinginevyo watozwe faini
kwa kushindwa kutekeleza agizo hilo muhimu la Serikali.
Pamoja na
kutembelea mnada huo Bi. Tellack pia alitembelea Kituo cha Afya cha
Wilaya ya Kishapu kilichoandaliwa kama sehemu maalumu ya kupeleka
wagonjwa wa corona endapo watabainika Wilayani humo kama hatua muhimu ya
kujionea ni namnagani Wilaya ya Kishapu imejipanga kukabiliana na
ugonjwa huo.
Akiwa katika
kituo hicho cha Afya Mkuu wa Mkoa amejionea vifaa vnitakovyotumiwa na
waudumu wa Afya kujikinga na kuwahudumia wagonjwa na kuwataka wahudumu
hao kuwa tayari kwa lengo la kukabiliana na kuhudumia wagonjwa hao kwa
tahadhari kubwa.
Mnada huo
unaowakutanisha wafanyabiashara wa mifugo kutoka sehemu mbalimbali za
mkoa wa Shinyanga na mikoa jilani ufanyika kila Siku ya Alhamisi na
kuvuta wafanyabiashara wa aina nyingine nje na ndani ya mnada huo ambao
pia wametakiwa kuchukua tahadhari kwa kuweka vitakasa mikono katika
maeneo yao ya biashara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...