Leandra Gabriel, Michuzi TV
MWAKA
1665 kulitokea mlipuko wa ugonjwa wa Tauni uliojulikana zaidi kama
"Black Death" nchini Uingereza hali iliyopelekea shule, vyuo na huduma
mbalimbali za kijamii kuzuiliwa kwa muda kwa lengo la kupunguza kasi ya
maambukizi ya Tauni kama inavyofanyika sasa ambapo dunia inakabiliwa na
mlipuko wa virusi vya Corona (Covid-19.)
Wakati
huo Isaac Newton alikuwa mwanafunzi Chuo Kikuu Cambridge na hakuwa
Profesa na alilazimika kurudi nyumbani kati ya mwaka 1665 na 1666 baada
ya Cambridge kufungwa kutokana na janga hilo.
Newton
alirejea Cambridge 1667 na nadharia zinazodumu hadi sasa hiyo ni baada
ya kutumia vyema muda huo ambapo janga hilo lilitokea.
Wakati
huo wa janga la Tauni "Babonic Plague", Newton akiwa nyumbani
alishuhudia tufaa likianguka toka mtini kwenye bustani ya familia huko
Woolsthorpe (maili 50 kutoka Cambridge). Hapo alijiuliza maswali
yaliyopelekea ugunduzi wa nadharia ya nguvu ya uvutano(Gravity).
Newton alifanya majaribio kadhaa ya mwanga ambayo pia yaliyopelekea kugundua nadharia ya Optiki.Vilevile Newton aliandaa njia na kanuni mpya katika fani ya hisabati na zikawa chimbuko la Calculus.
Janga hilo lilipelekea robo ya wakazi wa Uingereza kufariki kutokana na tauni iliyopiga kati ya miaka ya 1665 na 1666.
Newton
alirudi chuoni Cambridge mwaka 1667, akiwa na nadharia alizoziandaa
akiwa nyumbani, ndani ya miezi 6 tu alifanywa kuwa mtafiti na miaka
miwili alitunukiwa shahada ya Uzamivu katika Chuo Kikuu Cambridge.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...