Na Karama Kenyunko globu ya jamii. 
ASKARI Polisi wa Maabara ya uchunguzi wa Kisayansi kutoka Polisi Makao Makuu, Inspekta Fatuma Mbwana ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa,  maandishi ya maelezo ya Onyo ya mlalamikaji Diana Naivana , yanafanana na sampuli ya maandishi ya mshtakiwa Joyce Kitta ambaye ni askari.

Inspekta Fatuma ambaye ni shahidi wa kwanza katika kesi ya kushawishi rushwa ya sh milioni 200 inayowakabili askari upelelezi wanne wa kituo cha polisi Kawe, ameeleza hayo leo Aprili 6, 2020 mbele ya Hakimu ya Hakimu Mkazi Mwandàmizi Rashidi Chaungu ushshidi alipokuwa akitoa ushahidi wake.

Akiongozwa na wakili wa serikali Mogela Ndimbo,  kutoa ushahidi wake, shahidi huyo amedai Mei 16 mwaka jana akiwa maabara, alipokea barua kutoka Taasisi ya Kuzuia na kupokea Rushwa (TAKUKURU), makao makuu Dar es Salaam yenye vielelezo ambavyo ni karatasi ya maelezo ya onyo na sahihi za Diana ya Desemba 17 mwaka 2018 na Sampuli ya sahihi ya mshtakiwa Joyce akitakiwa avifanyie uchunguzi.

Amedai kuwa baada ya uchunguzi, alibaini kuwa sampuli ya maandishi ya Joyce inafanana na maandishi ya maelezo ya onyo yanayodaiwa kuwa ya Diana na yaliandikwa na mtu mmoja na kwamba uchunguzi huo pia umebaini sampuli za sahihi za Diana hazifanani na sahihi zilizo katika maelezo hayo ya onyo.

Ameendelea kudai kuwa, naada ya uchunguzi huo aliandaa ripoti na kuiwasilisha katika mamlaka iliyomtaka afanyie uchunguzi.

Mbali na Joyce washtakiwa wengine katika kesi hiyo ambao wote ni askari wa upelelezi  ni Emmanuel Njegele , Shaban Sillah na Ulimwengu Rashidi.

Wote kwa pamoja  wanakabiliwa na mashtakà manane yakiwemo ya kujihusisha na vitendo vya rushwa ambapo wanadaiwa kuwa, Desemba 17, 2018 maeneo ya Rainbow Social Club, Kinondoni, washtakiwa hao wakiwa maofisa wa upelelezi, waliomba rushwa ya Sh milioni 200 kutoka kwa Diana Naivasha kama kishawishi cha kutokuchukuliwa hatua za kisheria kwa kosa la kukutwa na nyara za serikali.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Aprili 15 mwaka huu. Itakapokuja kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa kwa shahidi wa pili wa upande wa mashtaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...