Mnamo tarehe 04 April 2020 kundi la Simba Jamii Tanzania " Ultras" lilikabidhi zawadi ya tank la maji la lita 2,000 pamoja na kifaa cha kuzalisha umeme Jua (Solar) kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Ukhty Raya kilichopo eneo la Mindu mkoani Morogoro.

Akikabidhi misaada hiyo mwakilishi wa Simba Jamii mkoani Morogoro Bwana Rashid "Wizzy" Mbegu alimfahamisha mlezi na msimamizi wa kituo hicho Bi Raya kuwa Simba Jamii itawakabidhi watoto wote wa kituo hicho pea 50 za viatu ilivyovipokea kutoka kwa wahisani wa nje ya nchi pamoja na kuangalia jinsi ya kuwasaidi kuwa na mradi utakaowaingizia kipato.

Kundi la Simba Jamii Tanzania  ambalo lina makazi yake Kinondoni Dar Es Salaam limekuwa likikabidhi misaada sehemu mbalimbali kwa watu ama taasisi zisizo na hali nzuri ya kiuchumi.

Kundi hilo lililochipukia ghafla toka kuanzishwa kwake miezi sita iliyopita tayari limeshakabidhi vifaa katika majumba ya ibada,vituo vidogo vya afya nk.

Kundi lipo chini ya uenyekiti wa Gabriel Samson Ntole na Katibu Mtendaji Severine Kasimba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...