Leo tarehe 05 April,2020 kundi maarufu la Simba Jamii Tanzania limekabidhi sehemu ya misaada ya viti vya walemavu (wheelchairs) kwa mwanafunzi mlemavu Lucy Furaha Kajuni wa shule ya Msingi Nzovwe iliyopo mkoani Mbeya.
Msaada huo ulitolewa mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya Shule hiyo Ndg Happy Bakamba pamoja na maafisa kadhaa wa Kata.
Simba Jamii iliwakilishwa na wanachama wake Ndg Jacob Madege,Ndg Mwakalilila,Ndg Anangisye na Ndg Maureen.
Mkuu wa msafara wa Simba Jamii Ndg Maureen amedai kuwa misaada hiyo ni sehemu ya misaada endelevu inayotolewa na Kundi la Simba Jamii kila kona ya Tanzania.
Na ametoa rai kwa makundi mengine ya whatsap kuwa mstari wa mbele kuisaidia jamii inayowazunguka kwani kufanya hivyo ni kumfurahisha Mwenyezi Mungu na kuleta umoja na upendo baina ya watanzania.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...