Na Emmanuel Massaka,Michuzi Tv.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga mkoani Pwani Abdallah Ulega amefanya ziara katika kata mbilimbali za jimbo hilo kwa lengo la kukagua miundombinu ya barabara ilivyoharibiwa  na mvua zinazoendelea kunyesha nchini.

Kutokana na uharibifu huo Ulega amemtaka Meneja wa Wakala wa Ujenzi wa Barabara Vijijini (TARURA) kutafuta namna ya kuhakikisha barabara hizo zinapitika.

Akizungumza hivi karibuni jimboni humo na baadhi ya wananchi wa kata hizo waliojitolea nguvu zao kurekebisha barabara hizo wakati wa ziara hiyo amewapongeza kwa kujitolea na kuwataka kuendelea kujitolea katika kazi mbalimbali za kijamii ili kuunga mkono kauli ya Rais Dk. John Magufuli ya Hapa Kazi Tu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkuranga Juma Abeid amesema halmashuri hiyo imetenga shilingi milioni 250 kutoka katika mapato yake ya ndani kwa ajili ya kufanya marekebisho ya barabara zilizoharibika kwa mvua.

Akifafanua zaidi Abeid amesema fedha hizo zitagawanywa katika kata zote 25 za wilaya hiyo ambapo kila kata itapata Sh.milioni 10.


Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi( Mb) wa Mkuranga,Abdallah Ulega (kushoto) akikagua daraja la Nyatanga katika Kijiji cha Mbulani kata ya Panzuo wilaya ya Mkuranga mkoa wa Pwani likiwa limesombwa na maji na kusababisha kukatika kwa mawasiliano katika ziara ya kukagua miundombini mbalimbali.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi( Mb) wa Mkuranga,Abdallah Ulega akishiriki njenzi wa barabra katika ziara kukagua miundombinu mbalimbali.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Hassan Sanga (kulia) akishiriki njenzi wa barabra katika ziara kukagua miundombinu mbalimbali.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...