
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na
Utawala, Issa Nchasi akiwakaribisha wataalamu wa Afya kutoa mafunzo juu
ya ugonjwa wa corona kwa watumishi wa Wizara ya Madini Makao Makuu
jijini Dodoma, leo asubuhi.


Mtaalamu wa afya Dkt. Shamza Said
akitoa elimu ya ugonjwa wa corona kwa watumishi wa Wizara ya Madini ili
kuwapa uelewa wa ugonjwa huo na namna ya kujikinga

Watumishi wa Wizara wakifuatilia mafunzo juu ya ugonjwa wa corona kutoka kwa wataalamu wa afya (hawapo pichani)

Mtaalamu wa mazingira katika
masula ya Afya, Koyi Veronika akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo
yaliyotolewa kwa watumishi ofisi za Wizara ya Madini Makao Makuu, jijini
Dodoma

Msaidizi wa Ofisi Mwandamizi,
Veneranda Charles akiuliza swali kwa wataalamu wa afya juu ya vitakasa
mikono vinavyoshauriwa kutumika ili kujikinga na ugonjwa wa corona.

Kamishna msaidizi wa Madini
anayeshughulikia masuala ya Ushiriki wa wananchi na ncchi katika uchumi
wa madini, Ngole akiuliza swali kwa wataalamu wa afya mafunzo hayo
yakiendelea.

Dkt. Shamza Said akijibu maswali juu ya ugonjwa wa Corona aliyoulizwa na watumishi.

Mkurugenzi wa Rasilimali watu na
Utawala, Issa Nchasi, akiwashukuru na kuwaaga wataalamu wa Afya mara
baada ya zoezi la kutoa mafunzo juu ya ugonjwa wa corona kwa watumishi
wa Wizara ya Madini Makao Makuu, kukamilika.
…………………………………………………………………………………………………………..
Asteria Muhozya na Nuru Mwasampeta – Dodoma
Watumishi wa
Wizara ya Madini wakiongozwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali
Watu, Issa Nchasi leo Aprili 2, wametembelewa na wataalamu wa afya kwa
lengo la kutoa elimu juu ya ugonjwa wa corona unaosababishwa na virusi
vya covid-19 na namna ya kujikinga na ugonjwa huo.
Wataalamu hao
ni pamoja na Dkt. Shamza Said ambaye ni miongoni mwa wataalamu wa afya
wanaojishughulisha na magonjwa yanayoambukiza kwa kasi aliyeambatana na
Toyi Veronica mtaalamu wa mazingira katika masuala ya afya.
Akizungumzia
virusi vinavyosababisha ugonjwa huo Dkt. Shamza alisema virusi vya
covid-19 ni virusi vipya kuwepo duniani vya aina hiyo vinavyotoka kwa
wanyama na kusababisha madhara kwa binadamu.
Amesema
virusi hivi pindi vinapoingia mwilini mwa binadamu vinasababisha madhara
mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushambulia mfumo wa upumuaji, figo, ini
na madhara mengine na kuwasihi watumishi na jamii pindi wanapohisi kuwa
na dalili za ugonjwa huo, kuhakikisha wanawahi katika vituo vya afya ili
kupatiwa huduma stahiki kabla ya ugonjwa kusababisha madhara makubwa
mwilini.
Amesema,
unapowahi kupata huduma za kitabibu kuna uwezekano mkubwa wa kupona
tofauti na mtu anayekwenda kutibiwa awapo katika hali mbaya.
Aidha, Dkt
Shamza amewashauri watumishi kupunguza mikusanyiko isiyokuwa ya lazima,
kunawa kwa sabuni na vitakasa mikono kila wakati, kuacha kukusanyika
katika masherehe, matumizi ya vifaa vya vyakula yasiwe shirikishi,
kuzingatia uvaaji sahihi wa mask pamoja na kuwa wawazi wanapojihisi kuwa
na maambukizi ya ugonjwa ili kuepusha kuambukiza watu wengine.
Kwa
kuhitimisha, Dkt. Shamza amewataka watumishi kutoa elimu ya corona kwa
watu wengine katika familia ndugu jamaa na marafiki ili elimu hii
iwafikie wengi na waweze kujikinga na hivyo kupunguza maambukizi nchini.
“Unapopata elimu, elimisha na wengine” amisisitiza Dkt. Shamza.
Kwa
kuhitimisha, Dkt. Shamza amewataka watumishi kutoa elimu ya corona kwa
watu wengine katika familia ndugu jamaa na marafiki ili elimu hii
iwafikie wengi na waweze kujikinga na hivyo kupunguza maambukizi nchini.
“Unapopata elimu, elimisha na wengine” alisisitiza.
Kwa upande
wake, Mtaalamu wa mazingira katika masula ya Afya, Koyi Veronika
ameushauri uongozi wa wizara kupunguza vikao kazi vya ana kwa ana na
badala yake uongozi kwa kushirikiana na wataalamu wa TEHAMA kuratibu
mfumo wa kutumia mtandao katika vikao vyao ili kuepusha maambukizo
miongoni watumishi.
Kwa
kuhitimisha, Dkt. Shamza amewataka watumishi kutoa elimu ya corona kwa
watu wengine katika familia ndugu jamaa na marafiki ili elimu hii
iwafikie wengi na waweze kujikinga na hivyo kupunguza maambukizi nchini.
“Unapopata elimu, elimisha na wengine” alisisitiza.
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Rasilimali watu na Utawala, Issa Nchasi amewashukuru
Wizara ya Afya kwa mpango mzuri walioanzisha wa kupita na kutoa elimu
kwa watumishi na kuahidi kuyasimamia yote waliyoelekeza ili kupambambana
na gojwa hatarishi la corona.
Baada ya
kutoa elimu hiyo zilipo ofisi zaWizara Makao Makuu, wataalamu hao
wameelekea zilipo ofisi za Taasisi ya Jiolojia na Utafiti na Ofisi ndogo
za Wizara ya Madini, Chuo cha Madini na kumalizia mafunzo hayo ofisi za
Tume ya Madini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...