NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO 

WAKAZI wa Kitongoji cha Ukuni Kata ya Dunda ,wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, wameunda Kamati Maalumu itayosimamia ukarabati wa miundombinu ya Barabara ambayo imekuwa kero kwa wananchi . 

Wakiwa katika kikao cha uundwaji wa Kamati hiyo, wajumbe wamejadiliana kwa kina kuhusiana na mchakato huo, unaolenga kuondokana na hali tete ya ubovu wa miundombinu hiyo iliyopo kwenye Kitongoji hicho, ambapo Kamati hiyo inatarajia kuanza kazi mara moja. 

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ukuni, Dawson Shigera, alisema kwa muda mrefu wakazi kitongojini hapo walikuwa wanakabiliana na uchakavu wa miundombinu ya barabara, na kwamba wamewasiliana na TARURA ambayo imedai inaifanyia kazi changamoto hiyo watakapopata fedha watafika kwa ajili hiyo. 

“Baada ya kutambua changamoto zetu na majibu ya wataalamu wa TARURA, tukaona utekelezaji wake utachukua muda mrefu kutokana na taratibu za utekelezaji wake, tukaitana na kuazimia kujichangisha kulingana na tayari tumekusanya shilingi laki nane na nusu sanjali na ahadi ya shilingi laki tatu, leo tumeunda Kamati itayosimamia zoezi hilo,” alisema Shigera. 

Wakizungumza baada ya kikao hicho, Makamu Mwenyekiti wa Kamati Dkt. Omary Omary alieleza,lengo la kamati ni kuhakikisha kitongoji kinakuwa katika mazingira mazuri , na changamoto ya miundombinu ya barabara inapoteza manzari ya kitongoji chao. 

Nae Doto Kwege alifafanua, katika sekta ya miundombinu ya barabara imekuwa na changamoto kubwa, ambapo wanafunzi wanakabiliwa na hali ngumu waendapo na kurudi kutoka shule, na kwamba wanatarajia kero hiyo itapungua kama si kumalizika kabisa.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...