Dkt.
Grarvin Kweka wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akionesha namna ya
kutumia vitakasa mikono kwa wafanyakazi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)
juu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona (Covid 19) wakati
wa mafunzo yaliyoandaliwa na kufanyika katika ofisi za Bodi hiyo Jijini
Dar es Salaam.
Dkt. Grarvin Kweka wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili akitoa mada ya namna ya kujikinga na virusi vya Corona kwa wafanyakazi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) juu
ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona (Covid 19) wakati wa
mafunzo yaliyoandaliwa na kufanyika katika ofisi za Bodi hiyo Jijini Dar
es Salaam.
Wafanyakazi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) wakifuatilia kwa umakini mafunzo yaliyotolewa na madaktari juu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona (Covid 19) na virusi vya Ukimwi. Mafunzo yaliandaliwa na kufanyika katika ofisi za Bodi hiyo Jijini Dar es Salaa
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Wafanyakazi
wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) wamepatiwa mafunzo ya jinsi ya
kujikinga na maambukizi ya virusi vya CORONA ili kumpa fursa mtumishi
kujua hali yake na hivyo kuchukua hatua zaidi za kujilinda na kuwalinda
wengine.
Mafunzo hayo
yameendana sambamba na upimaji kwa hiari wa HIV, Homa ya Ini, Shinikizo
la Damu, kisukari Kisukari na ulinganifu wa urefu na uzito yaliyofanyika
kwa siku moja ndani ya Ofisi za TTB Jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi
wa TTB, waliweza kupata elimu hiyo muhimu pamoja na namna ya
kukabiliana na msongo wa mawazo ili kufanya kazi kwa ufanisi na kuongeza
tija kwa shirika na taifa kwa ujumla.
Katika
mafunzo hayo, mada zilitolewa na Wataalam wa Afya kutoka Hospitali ya
Taifa Muhimbili Dkt. Garvin Kweka kwa kushirikiana na Dkt. Hafidh Ameir
wa Tanzania CommisionCommission for AIDS (TACAIDS).
Kwa
pamoja madokta hao, walitoa elimu inayowataka wafanyakazi hao kujikinga
na maambukizi ya virusi vya Corona ambapo Shirika la Afya la Dunia
(WHO) limetangaza kama janga la dunia na takribani watu milion
2,416,135 wamepata maambukizi, waliopona ni 632,983 na vifo ni 165,939
kwa dunia nzima.
Wafanyakazi wa TTB Wametakiwa kujikinga na kuwakinga wengine wakiwa wanatoa huduma kwa jamii pamoja na jamii inayowazunguka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...