Na Leandra Gabriel, Michuzi TV
NAHODHA
na mabaharia sita wa kichina ambao ni Lin Xinyong, Zoa Yongzian, Tan
Yian, Xie Wenbin, Xu Kun na Mu Yong wamekutwa na hatia ya kujaribu kuua
watanzania wawili mwezi uliopita kwa kuwatupa baharini kwa kile
kilichoelezwa kuwa wangeweza kuwaambukiza Virusi vya Corona (Covid -19.)
Aidha
mahakama hiyo imemuhukumu nahodha wa meli hiyo iliyokuwa inatoka Durban
nchini Afrika Kusini Captain.Rongli kulipa faini ya Euro 4350 na kila
baharia ametozwa Euro 2173.
Aidha
Rongli ametozwa faini ya Euro 2175 kwa usimamizi mbovu na Euro 435 kwa
kutoripoti uzamiaji uliofanywa na vijana hao na kuelekezwa kwenda jela
miaka minne asipolipa faini.
Amiri
Salamu (20) na Hassani Rajabu (30) walitoswa baharini baada ya kupewa
life jacket na chupa mbili za maji pekee na baada ya siku mbili
walijikuta katika fukwe wa utalii wa Dusk, kwa Zulu Natal kilomita 50
kutoka Kaskazini mwa Durban. Ambapo walioelekwa hospitali ambapo
waaligundulika kuugua njaa, kiu na kuishiwa nguvu.
Imeelezwa
kuwa mabaharia walikiri mashtaka hayo huku nahodha wa meli hiyo Rongli
akikiri makosa hayo ya usafirishaji yanayohusiana na kuhatarisha maisha
ya watu.
Aidha msemaji
wa Mamlaka ya mashtaka ya kitaifa (NPA) Natasha Kara amesema kuwa chombo
hicho kiliondoka Durban Machi 26 na siku iliyofuata kuligundulika kuwa
na wanaume wawili wa kitanzania ambao ni wazamiaji ambao waliombwa
wajitambulishe na kueleza kuwa walikataa kuvaa barakoa.
Aidha
amesema kuwa kabla ya kutoswa baharini walipatiwa maji na vyakula na
kutengwa kwenye chumba tofauti kwa kuwa hali yao ya Covid -19
haikufahamika.
Kabla ya
kutoa hukumu hiyo Kaimu hakimu wa mahakama Vishalan Moodley alieleza
kuwa tuhuna hizo ni za majaribio ya mauaji na utekelezaji mbaya wa
majukumu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...