WAUMINI wa Dini
ya Kiislam wakiwa katika Ibada ya kuusalia Mwili wa Marehemu Marin
Hassan Marin, Mwandishi wa Habari Muandamiziu wa Shirika la Utangazaji
Tanzania (TBC) sala na dua hiyo imefanyika katiuka Msikiti wa KMKM
Kibweni Wilaya ya Magharibi”A” Unguja leo 2/4./2020,saa nne na kuzikwa
katika Makaburi ya Mwanakwerekwe Jijini Zanzibar.

WAUMINI wa Dini
ya Kiislam wakiuombea dua mwili wa Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa
Shirika la Habari Tanzania (TBC) baada ya kumalizika Sala ya Maiti
iliofanyika katika Msikiti wa KMKM Kibweni Jijini Zanzibar

MKURUGENZI Mkuu
wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Ayoub Rioba akizungumza na
kutowa shukrani baada ya maziko ya Mfanyakazi wake Mwadishi Muandamizi
Marehemu Marin Hassan Marin, yaliofanyika katika makaburi ya
mwanakwerekwe Jijini Zanzibar.

WAZIRI wa
Habaro Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar.Mhe. Mahmoud Thabot Kombo
akizungumza na kutowa shukrani kwa niaba ya Wizara yake wakati wa hafla
ya maziko ya Mwandishi wa Habari Muandamizi Tanzania Marehemu Marin
Hassan Marin, yaliofanyika katika makaburi ya Mwanakwerekwe Jijini
Zanzibar

MWAKILISHI wa
Familia ya Marehemu akitowa neno la shukrani kwa Serikali ya Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa ushirikiano
wao katika kufanika msiba huo.


MAWAZIRI wa
Habari wa SMT na SMZ. Kushoto Waziri Habari Utalii na Mambo ya Kale
Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe, wakiwasili katika viwanja vya
Msikiti wa Kibweni KMKM kuhudhuria maziko ya Mwandishi wa Habari
Mwandamizi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Marin Hassan Marin,
yaliofanyika leo 2/4/2020 na kuzikwa katika makaburi ya Mwanakwerekwe
Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.


WANANCHI
wakibeba Jeneza lililokuwa na Mwili wa Marehemu Marin Hassan Marin,
wakitoka nyumbani kwa marehemu na kuelekea katika Msikiti wa Kibweni
KMKM kwa ajili ya kuombea dua kwa ajili ya maziko yaliofanyika katika
makaburi ya Mwanakwerekwe Jijini Zanzibar.

WAUMINI na
Wananchi wakishiriki katika kisomo cha Hitma na Dua kumuombea Marehemu
Marin Hassan Marin, iliofanyika nyumbani kwao Kibweni Wilaya ya
Magharibi “B” Unguja wakati wa hafla hiyo ya maziko yaliofanyika leo
2/4/2020 saa nne asubuhi na kuzikwa katika makaburi ya Mwanakwerekwe
Jijini Zanzibar.(Picha na Othman Maulid)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...